Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Hatimaye mtandao umerejea nchini Tanzania baada ya kufinywa kwa siku sita.
Hili limehjiri baada ya Rais Samia kuapishwa na kuchukua majukumu yake rasmi.
Katika hotuba aliyotoa wakati wa kuapishwa kwake Rais Samia alitoa maagizo kwa vyombo vya usalama kuhakikisha hali imerejea kama kawaida kwa Watanzania.
“Kamati ya kitaifa na kamata za ulinzi za mikoa na wilaya nawataka muhakikishe, kuanzia leo maisha ya wananchi yanarejea mara moja,” alisema Rais Samia.
Kuzimwa wa mtandao kulifanya mawasiliano kuwa magumu, biashara zimesimama, sekta ya utalii imedorora na hata kuwa vigumu kujua hali inavyoendelea nchini humo Tanzania.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.