Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2025: Rais wa Kenya William Ruto ampongeza rais Samia Suluhu kwa ushindi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

gg

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto, ametuma salamu za pongezi kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kufuatia kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Rais Ruto amewataka wananchi wa Tanzania kudumisha amani na kuheshimu utawala wa sheria.

Aidha, alihimiza wadau wote wa kisiasa na jamii kuchukua hatua za kujadiliana kwa heshima na kuvumiliana ili kutatua changamoto zozote zinazoweza kujitokeza, kwa lengo la kulinda demokrasia na kudumisha uthabiti wa taifa.

Rais Ruto alisisitiza kuwa Kenya iko tayari kuendeleza ushirikiano wa karibu na Tanzania katika kutimiza ndoto ya pamoja ya Afrika Mashariki yenye amani, ustawi, na mshikamano.

“Kwa niaba ya Serikali ya Kenya, nawapongeza kwa dhati Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha uchaguzi huu kwa njia ya kidemokrasia. Ushirikiano wetu utaendelea kuimarika kwa manufaa ya wananchi wetu na ustawi wa eneo zima la Afrika Mashariki,” alisema Rais Ruto.

Malori ya mizigo ya Kenya yazuiwa kuingia Tanzania kupitia mpaka wa Namanga

.

Wafanyabiashara kutoka Kenya wamepata pigo kubwa kufuatia vurugu za uchaguzi mkuu zilizotokea nchini Tanzania.

Hii ni baada ya idara ya uhamiaji ya Tanzania kupiga marufuku magari yote ya usafiri wa abiria na Mizigo kuingia nchini Tanzania.

Katika mpaka wa Namanga,foleni ndefu ya malori kutoka Nairobi Kenya imeendelea kushuhudiwa baada ya kukatazwa kuingia Tanzania.

Ghalib Ahmed dereva wa Lori la mizigo kutoka Nairobi Kenya anaenunuwa machungwa nchini Tanzania na kusambaza jijini Nairobi amekwama mpakani kwa karibu wiki sasa.

“Mimi hununuwa machungwa Tanzania na kuuza Nairobi,lakini tangu uchaguzi uchaguzi ulipofnayika wametukataza kuingia wakidai tunaweza kuwa na dhamira mbaya, siwezi kurudi Nairobi nitapata hasara ya mafuta, nasubiri kuangalia iwapo watafungua mpaka Samia akiapishwa.”alisema.

Maafisa wa forodha katika mpaka wa Namanga wanasema hiyo ni amri kutoka uongozi kwa ajili ya usalama.

Upande wa usafiri wa umma, Kampuni za mabasi ya usafiri wa abiria kama vile Tahmeed,Modern Coast na nyinginezo zinazosafirisha abiria kutoka Kenya hadi Tanzania pia zimekadiria hasara kubwa baada ya usafiri huo kusimamishwa kwa zaidi ya siku 6 sasa.

Leila Menza, mhudumu wa kukata nauli za mabasi ya umma kutoka Nairobi anasema, wanatumai baada ya Samia kuapishwa hii leo, shughuli zitarejea katika hali ya kawaida waendelee na safari hapo kesho” alimalizia.

Katika mpaka huu wa Namanga, upande wa uchukuzi ,wafanyabiashara wa malori ya mizigo kutoka Kenya ndio waliothirika zaidi na kusitishwa kwa shughuli za kazi baada ya uchaguzi wa Tanzania.

Kwa kawaida,kila siku mpaka wa Namanga hupitish malori mia 3 kutoka na kuingia Tanzania kwa uchukuzi wa bidhaa mbalimbali.

Sherehe ya kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu yaanza

Gwaride la Jeshi la Tanzania
Maelezo ya picha,Gwaride la Jeshi la Tanzania kutumbuiza katika hafla ya uapisho wa rais mteule

Hafla ya kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan imeanza katika uwanja wa kijeshi lakini raia wa kawaida hawatahudhuria.

Rais mteule wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuapishwa wakati wowote kutoka sasa baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Jumatano uliokumbwa na utata.

Viongozi mbalimbali barani Afrika wamehudhuria ni pamoja na Naibu rais wa Kenya Kindiki Kithure, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud , Rais wa Burundi Hakainde Hichilema na wanadiplomasia.

Sherehe hizi zinafuata itifaki za kijeshi.

Kilele cha sherehe ni kiapo cha uongozi na mizinga 21 kufyatuliwa.

Ni mara ya kwanza kwa rais mwanamke kula kiapo baada ya kushinda uchaguzi nchini Tanzania.

Kuwepo kwa gwaride kunaashiria mamlaka ya rais ambaye pia atakuwa amri mkuu wa majeshi.

Hata hivyo, upinzani umeutaja uchaguzi wa 2025 uliofanyika juma lililopita kama kejeli kwa demokrasia.

Hafla hiyo inafanyika katika uwanja wa kijeshi na haitakuwa wazi kwa umma.

Picha ambazo BBC imezipata ni gwaride la jeshi tayari liko uwanjani kwa shughuli hiyo nzima ikitarajiwa kutumbuiza wageni mashuhuri watakaokuja kushuhudia uapisho wa rais mteule Samia.

TBC inapeperusha matangazo hayo mubashara kutoka Dodoma kwa taifa.

Rais Samia alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29 kwa kujinyakulia asilimia 97.66 ya jumla ya kura zote zilizopigwa.

INEC imetangaza kwamba ushindi mkubwa wa Rais Samia ambao haujawahi kushuhudiwa nchini Tanzania katika awamu tano za kwanza za uongozi wa nchi hiyo.

Wapiga kura milioni 37 walisajiliwa kushiriki kwenye uchaguzi wa mwaka huu huku INEC ikisema kwamba Samia alipata jumla ya kura milioni 31.

Aidha tume hiyo imesema pia kwamba asilimia 87 ya waliosajiliwa kupiga kura walijitokeza kushiriki kwenye uchaguzi huo ambao ulishuhudia maandamano huku mji wa Dar es Salaam ukikabiliwa na amri ya kutotoka nja kati ya saa 12 jioni na saa 12 asubuhi.

Tayari Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ameapishwa baada ya kumshinda mpinzani wake wa chama cha ACT-Wazalendo Othman Masoud.

Sherehe hiyo ya uapisho wa rais wa Zanzibar ilihudhuriwa na maafisa wakuu wa serikali, akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango, wanadiplomasia, na maelfu ya raia wa Zanzibar.

Samia ashinda uchaguzi Tanzania huku mamia wakihofiwa kufariki katika maandamano

Wageni wahudhuria uapisho wa urais lakini raia wa kawaida hawajaruhusiwa
Maelezo ya picha,Wageni wahudhuria uapisho wa urais lakini raia wa kawaida hawajaruhusiwa

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment