Israel yairejesha miili 45 ya wapalestina mjini Gaza

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Israel yairejesha miili 45 ya wapalestina katika Ukanda wa GazaPicha: Abed Rahim Khatib/Anadolu/picture alliance

Wizara ya afya inayoendeshwa na wanamgambo wa Hamas Gaza, imesema Israel imerejesha miili 45 ya wapalestina na kufikisha idadi jumlya ya miili iliyorejeshwa kuwa 270, tangu kufikiwa makubaliano ya usitishwaji mapigano.

Chini ya makubaliano hayo yaliyosimamiwa na rais wa Marekani Donald Trump, Israel ilipaswa kurejesha miili ya wapalestina 15 kwa kila mwili wa mateka mmoja utakaorejeshwa kutoka Gaza.

Israel imethibitisha kwamba miili iliyotolewa na wanamgambo wa Hamas hapo jana ni ya mateka watatu waliochukuliwa wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7.

Kwengineko Waziri wa usalama wa taifa Israel amesema polisi nchini humo imemkamata mwanasheria wa zamani wa kijeshi nchini humo Yifat Tomer-Yerushalmi, kufuatia sakata la kuvujisha  vidio iliyowaonyesha wanajeshi wa Israel wakiwanyanyasa wafungwa wa kipalestina.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment