Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwa na mwenzake wa Urusi Mikhail Mishustin.Picha: Dmitry Astakhov/AP Photo/picture alliance
Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema nchi yake inataka kuimarisha mahusiano yake na Urusi na kutetea masilahi yao ya pamoja ya kiusalama.
Aliyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Urusi nchini humo Mikhail Mishustin. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika mjini Hangzhou, Li amesema Urusi na China ni marafiki na washirika wazuri wanaoaminiana.
Mishustin yupo katika ziara ya siku mbili China ambako shirika la habari la taifa TASS limesema hapo kesho waziri mkuu huyo atakuwa na mazungumzo na rais Xi Jinping.
Mazungumzo yao yanatarajiwa kutuwama katika masuala ya Uchumi na ushirikiano wa teknolojia, wakati Urusi ikijaribu kukabiliana na vikwazo vya Magharibi kufuatia vita vyake Ukraine na China nayo ikivutana na Marekani kuhusu masuala ya kibiashara na kiteknolojia.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.