Raia Samia akabidhiwa cheti cha urais, akosoa maandamano

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa cheti cha ushindi wa urais baada ya kutangazwa mshindi kwa asilimia 98 ya kura.Picha: Sudi Mnette/DW

Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa cheti ushindi wa Urais wa Tanzania saa kadhaa baada ya Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo kutangaza kuwa amechaguliwa kwa kupata asilimia karibu 98 ya kura.

Unachohitaji kujua

  • Samia akabidhiwa cheti cha urais, akosoa maandamano
  • Rais Mwinyi aapishwa kwa muhula wa pili wa miaka mitano
  • Samia atangazwa mshindi wa Urais kwa asilimia 98 ya kura 
  • Hakuna nguvu kupita kiasi iliyotumika dhidi ya waandamanaji
  • UN yaitaka Tanzania kutotumia nguvu dhidi ya raia wake 

Rais Samia Suluhu Hassan akabidhiwa cheti cha ushindi wa urais

Hafla ya kukabidhiwa cheti hicho imefanyika makao makuu ya tume hiyo huko mji mkuu wa Tanzania, Dodoma.  na mwenyekiti wa Tume Huru ya uchaguzi Tanzania INEC, Jacobs Mwambegele.

Mapema leo Jumamosi, Tume hiyo ilimtangaza Rais Samia kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa asilimia 98 ya kura,katika uchaguzi uliokumbwa na maandamano yaliyojaa vurugu kote nchini humo.

Baada ya kupokea cheti hicho kutoka kwa mwenyekiti wa Tume Huru ya uchaguzi Tanzania INEC, Jacobs Mwambegele, kiongozi huyo aliyakosoa maandamano yaliyopinga zoezi la uchaguzi na ambayo yaliitikisa Tanzania kwa siku tatu mfululizo. 

Rais Samia Suluhu Hassan akionyesha cheti chake cha Urais baada ya kukabidhiwa na INECPicha: Sudi Mnette/DW

“Tunavishukuru vikosi vya usalama kwa kuhakikisha kuwa vurugu hazikuzuwia upigaji kura. Serikali ikalaani machafuko yaliyotokea,” alisema rais Samia akiongeza kuwa matukio hayakuwa yakizalendo hata kidogo. 

Samia aliingia kwa mara ya kwanza madarakani baada ya kifo cha mtangulizi wake John Pombe magufuli kilichotokea mwezi Machi mwaka 2021. 

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yamesema yalishuhudia wivi la vurugu za kutisha  katika taifa hilo la Afrika Mashariki kabla ya uchaguzi huo kufanyika ikiwemo kutekwa kwa wanasiasa wa ngazi ya juu kulikokithiri katika dakika za mwisho kabla ya zoezi hilo la Oktoba 29.

INEC yamtangaza rais Samia mshindi katika uchaguzi wa urais uliojaa vurugu

Matokeo hayo yanampa nafasi rais Samia aliyechukua madaraka kwa mara ya kwanza mwaka wa 2021, baada ya kifo cha mtangulizi wake John Pombe Magufuli, muhula mwengine wa pili wa miaka mitano kuiongoza nchi hiyo ya Afrika Mashariki iliyo na idadi ya watu milioni 68.

Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania INEC Jacob Mwambegele, aliyemtangaza Rais Samia mshindi wa urais wa Oktoba 29 kwa kujizolea asilimia 98 ya kuraPicha: INEC Tanzania

Maandamano yalizuka saa kadhaa, wakati watanzania walipokuwa wanaendelea na zoezi la kupiga kura Oktoba 29, kumchagua rais, wabunge na madiwani. Waandamanaji walimiminika barabarani kuupinga uchaguzi huo ambao haukuvishirikisha vyama vikuu viwili vya upinzani, CHADEMA na ACT Wazalendo. 

Baadhi yao walichoma moto vituo vya polisi, vituo vya mafuta, huku wakionekana barabarani wakisema kwa sauti kwamba hawakitaki chama cha CCM. Hapo jana (30.10.2025), chama kikuu cha upinzani CHADEMA kilidai watu takriban 700 waliuwawa katika ghasia za baada ya uchaguzi zilizoikumba nchi hiyo kwa siku tatu mfululizo. 

Hata hivyo Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo amekanusha madai hayo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment