Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Waziri mkuu mpya wa Japan Sanae Takaichi (kushoto) na rais wa China Xi Jinping (Kulia)Picha: Kaname Yoneyama/AP Photo/picture alliance
Waziri mkuu mpya wa Japan Sanae Takaichi amesema leo kuwa ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu Bahari ya Kusini ya China, Hong Kong na Xinjiang katika mkutano wa kwanza aliouita wa wazi na Rais wa China Xi Jinping.
Takaichi amesema katika mkutano wake na Xi pembezoni mwa mkutano wa kilele wa kila mwaka wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya nchi za Asia-Pasifiki, APEC, alimwambia rais huyo ya China kwamba anataka uhusiano wa kimkakati na wenye manufaa kati ya Japan na China.
Hata hivyo, amewaambia waandishi wa habari kuwa pia aliibua masuala kadhaa tata na kiongozi huyo wa China, akisema ni muhimu kwao kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja na ya wazi.
Kulingana na vyombo vya habari vya serikali , Xi alimwambia Takaichi ambaye ni waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Japan kwamba anatumai serikali yake itakuwa na “uelewa sahihi” wa nchi yake.
Ukraine yaitaka EU kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za Urusi
Ukraine imesema leo kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kuongeza ushuru kwa bidhaa za Urusi kama haiwezi kuzipiga marufuku kabisa, licha ya wasiwasi wa Ukraine juu ya uwezo wa Moscow kuendelea kufadhili uvamizi wake.

Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: Tetiana Dzhafarova/AFP
Umoja wa Ulaya wenye wanachama 27 umepunguza uagizaji wa bidhaa za Urusi kwa karibu asilimia 90 tangu uvamizi wake nchini Ukraine mnamo Februari 2022, lakini baadhi ya nchi bado zinaagiza mafuta na gesi, pamoja na kiwango kidogo cha chuma na mbolea.
Wakati wa mkutano na waandishi habari wa waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Andriy Sybiga uliohudhuriwa pia Rais Volodymyr Zelensky, Sybiga alisema wataibua suala hilo la kuwekewa kwa ushuru dhidi ya aina hiyo ya bidhaa.
Mataifa yote ya EU yapaswa kuunga mkono ushuru mpya dhidi ya Urusi
Umoja wa Ulaya unaweza kuongeza baadhi ya ushuru kwa Urusi ikiwa hatua hiyo itaungwa mkono na mataifa mengi bila ya haja ya wanachama wote kukubaliana, lakini kuwekwa kwa vikwazo vipya kunahitaji idhini ya pamoja kutoka kwa wanachama wote.
UN: Mamia ya watu huenda waliuawa El- Fasher
Mamia ya raia wa Sudan na wapiganaji wasio na silaha huenda wameuawa wakati kundi la RSF lilipouteka mji wa El- Fasher. Haya yamesemwa leo na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Wapiganaji wa RSF wakimkata mwenzao anayejulikana kama Abu Lulu kwa madai ya unyanyasajiPicha: Rapid Support Forces (RSF)/AFP
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva, msemaji wa Ofisi ya Haki ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema wanakadiria idadi ya vifo vya raia na wale waliotekwa wakati wa uvamizi huo wa RSF na njia za kutoka mjini huo huenda ikafikia mamia na kuelezea ushahidi wa mauaji makubwa ya kiholela.
Kuna ushahidi wa kubakwa kwa watu wasioungua wanawake 25
Magango amesema ofisi hiyo imepokea ushuhuda kutoka kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada kwamba watu wasiopungua wanawake 25 walibakwa na magenge wakati wapiganaji wa RSF walipoingia kwenye kambi za watu waliopoteza makazi yao karibu na chuo kimoja kikuu.
Pia amewaambia waandishi wa habari kwamba mashuhuda wamethibitisha kuwa wapiganaji wa RSF waliwachagua wanawake na wasichana na kuwabaka kwa makundi wakiwa wamewaelekezea bunduki, na kulazimisha takriban familia 100 zilizopoteza makazi kuondoka eneo .
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.