Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2025: Matokeo ya awali yaendelea kutangazwa

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania inaendelea kutangaza matokeo ya awali ya urais ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika 29 Oktoba, 2025.

Matokeo hayo yamepokelewa kutoka maeneo bunge mbalimbali.

Kulingana na matokeo ya awali yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Uchaguzi, yanaonyesha kuwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan yuko kifua mbele.

INEC ilikuwa imesema kuwa itamtangaza mshindi wa urais ndani ya saa 72 baada ya uchaguzi kufanyika 29/10/2025.

Uchaguzi Tanzania 2025: Mtandao waendelea kuminywa kwa siku ya tatu mfululizo

.

Mtandao umeendelea kuminywa nchini Tanzania kwa siku ya tatu na kufanya mawasiliano kuwa magumu.

Hapo jana, ulionekana kurejea kwa muda kidogo tu kama takriban saa moja hivi kabla ya kuanza tena kuminywa.

Hatua hii imefanya hata mawasiliano katika mitandao ya kijamii kuathirika na hivyo kufanya iwe vigumu vile vile kujua hali inavyoendelea nchini humo.

Jana, 30/10/2025, maandamano yalishuhudiwa kwa siku ya pili mfululizo na kusababisha vurugu na ghasia.

Baaadhi ya barabara pia zilikuwa zimewekwa vizuizi.

Nchi kama vile Marekani na Uingereza zilitoa tahadhari ya usafiri kwa raia wake wanaoishi nchini humo.

Ubalozi wa Marekani waonya raia wake kuwa usafiri wa barabarani unahatarisha maisha yao

.

Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhari kwa raia wake wanaoishi nchini Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa kwenye tovuti ya ubalozi huo na kusema kuwa Tanzania imekumbwa na maandamano ya nchi nzima na kusababisha “vurugu na vizuizi vya barabarani.”

Aidha, imeongeza kuwa kusafiri kwa barabara kuna hatarisha maisha yao.

Ufikiaji wa mtandao bado umekuwa na jambo gumu na kufanya mawasiliano yote kuwa magumu.

Aidha, ubalozi huo umesema kuwa safari za ndege nyingi za kimataifa zimefutwa na kushauri raia wake kuthibitisha safari zao kwanza kwa njia ya simu kabla ya kusafiri kuelekea uwanja wa ndege.

Ubalozi huo umewataka raia wake kuepuka maandamano, maeneo yenye mkusanyiko wa watu, kuepuka kujitokeza hadharani, kufuatilia taarifa za vyombo vya habari pamoja na kufahamu mazingira walioko.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment