Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Fundi ni mtu anayebeba ujuzi na ubunifu unaohitajika kila siku kwenye maisha yetu.
Aina ya fundi ” fundi kujenga,bomba,nguo, seremala,simu,kuchomerea,nk. Unapaswa kuzingatia haya kwenye kazi yako.
1. KUWA MWAMINIFU
Weka uaminifu mbele. Usiahidi kitu ambacho huwezi kukamilisha. Uaminifu hujenga wateja wa kudumu. Acha kutoa ahadi zisizotimizwa hii itakupotezea wateja wengi sana.
…
2. FANYA KWA UBORA
Usifanye kazi kwa haraka haraka. Ubora wa kazi yako ndiyo tangazo lako bora zaidi.
Kazi yako ikiwa na ubora unaohitajika sokoni utapata watu wengi sana.
…
3. FUATA MAELEZO YA MTEJA
Mteja akitoa maelekezo, sikiliza kwa makini. Hii huondoa kurudia kazi na inaleta kuridhika kwa mteja. Usifanye uonavyo wewe ila kile anachosema mteja wako.
…
4. KUWA NA NIDHAMU YA MUDA
Wasilisha kazi kwa wakati uliokubaliana. Mteja akiamini unaweza kuaminika kwenye muda, atakutafuta tena na tena.
Usiseme aje kuchukua kazi yake saa 6 mchana na wakati huwezi kutimiza kwa muda huo.
…
5. TUMIA VIFAA NA MALIGHAFI BORA
Vifaa duni vinaweza kuharibu kazi na jina lako. Bora utumie malighafi za ubora ili kazi idumu na ikusifie kwa watu wengi sana.
Hii itakutengenezea jina haraka sokoni.
6. KUWA NA MAWASILIANO BORA KWA MTEJA.
Mueleze mteja hatua unazochukua na gharama zote mapema. Mawasiliano mazuri huzuia migongano. Acha kujibishana au kujibu vibaya kwa mteja wako.
…
7. JIFUNZE KILA SIKU
Ujuzi wa fundi huongezeka kwa kujifunza. Fuata teknolojia mpya, mitindo mipya na mbinu za kisasa ili usibaki nyuma. Maarifa yatakusaidia Kuteka soko la wateja na kukufuata wewe tu.
Ni kitu gani ambacho uliwaki kukipata ulivyoenda kwa fundi na unatamani wengine waache.?
Niandikie hapa chini kwenye comment ili tuweze kujifunza pamoja.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.