Hamas yarejesha mabaki ya mateka wawili wa Israel

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

abaki ya mateka wa Israel Geisel Yossi Sharabi yakirejeshwa kutoka GAZAPicha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance

Jeshi la Israel limesema kundi la Hamas limerejesha mabaki ya mateka wawili zaidi wa nchi hiyo.

Jeshi hilo limesema miili hiyo miwili ilikabidhiwa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu katika ukanda wa Gaza na kisha ilisafirishwa na vikosi vya Israel hadi kwenye Taasisi ya Taifa ya Utaalamu wa Matibabu kwa ajili ya utambuzi.

Mabaki ya mateka wa Israel yatambuliwa

Jana jioni, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, alisema mabaki hayo yametambuliwa kuwa ya Sahar Baruch na Amiram Cooper, ambao wote walitekwa wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7, mwaka 2023 yaliofanywa na Hamas dhidi ya Israel.

Kufikia sasa, Hamas imesharudisha miili ya mateka 17 tangu kuanza kwa makubaliano ya kusitisha  mapigano, huku wengine 11 wakiwa bado wanashikiliwa Gaza na kupangiwa kurejeshwa chini ya masharti ya makubaliano.

Kiongozi wa China Xi Jinping amewaambia leo viongozi wa mataifa ya kanda ya Asia na Pasifiki kwamba nchi yake itasaidia kulinda biashara huria duniani.

Rais wa China, Xi JinpingPicha: Sergei Bobylev/Sputnik/AP Photo/picture alliance

Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo kwenye mji wa kusini mwa Korea Kusini wa Gyeongju, Xi amesema dunia inapitia kipindi cha mabadiliko ya haraka, na hali ya kimataifa inazidi kuwa tete.

Ameelezea matumaini ya kufanya kazi na nchi nyingine kupanua ushirikiano katika viwanda vya nishati safi.

Waziri wa fedha wa Marekani Scott Bessent, ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Trump, amesema hatua ya Marekani ya kusawazisha mahusiano yake ya kibiashara zitahakikisha haki na usawa kwa kila nchi.

Shambulizi la Urusi nchini Ukraine lawajeruhi watu 11

Urusi imefanya mashambulizi ya usiku kucha katika mji wa Sumy kaskazini mashariki mwa Ukraine na kuwajeruhi wakazi 11 ikiwemo watoto wanne. Hayo yamesemwa leo na huduma za dharura za Ukraine.

Shambulizi la Urusi katika mji ya Sumy nchini UkrainePicha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS

Kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye  mtandao wa Telegraph, kitengo hicho cha huduma za dharura kimesema shambulizi hilo la Urusi lililenga jengo la makazi la ghorofa, nyumba binafsi pamoja na miundombinu.

Gavana wa eneo hilo Ihor Kalchenko, amesema Urusi ilikuwa imeshambulia pia karakana ya reli na kuharibu mabehewa kadhaa na majengo.

Eneo hilo la Sumy linapakana na Urusi na limekuwa chini ya mashambulizi ya mara kwa mara ya droni na makombora.

RSF: Tumewakamata wapiganaji wanaoshtumiwa kwa unyanyasaji

Kikosi cha RSF nchini Sudan kimesema kimewakamata wapiganaji kadhaa wanaotuhumiwa kufanya unyanyasaji wakati wa kutekwa kwa mji wa El-Fasher.

Wapiganaji wa RSF nchini Sudan wakisherehekea katika barabara za El- FasherPicha: Rapid Support Forces (RSF)/AFP

Katika taarifa iliyotolewa jana jioni, RSF imesema imewashikilia wapiganaji kadhaa wanaotuhumiwa kwa ukiukaji uliotokea wakati wa kile ilichokiita ukombozi wa mji huo wa El- Fasher, ikiwa ni pamoja na mmoja anayejulikana kama Abu Lulu ambaye alionekana kwenye video nyingi kwenye mtandao wa TikTok akifanya mauaji ya kiholela.

Kundi hilo pia limethibitisha kufuata kwake “sheria, kanuni za maadili na nidhamu ya kijeshi wakati wa vita.”

Mauaji makubwa yaripotiwa kufanyika El- Fasher

Wakati huo huo, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Tom Fletcher, ameliambia Baraza la Usalama kwamba kulikuwa na ripoti za kuaminika za mauaji makubwa baada ya RSF kuingia El-Fasher.

Fletcher amesema RSF inadai kuwajibika lakini anatilia shaka kujitolea kwake huku kukiwa na habari za kutisha kutoka Darfur Kaskazini.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment