Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

By : Cantona Joseph|RFA

Wafanyakazi wa umma na wanafunzi nchini Tanzania wametakiwa kubakia nyumbani, baada ya ghasia za baada ya uchaguzi kushuhudiwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushinda uchaguzi huo.
Unachohitaji kujua.
- Watanzania waamriwa kubakia nyumbani kufuatia ghasia zinaziendelea
- Polisi yatangaza amri ya kutotoka nje Dar es Salaam
- Wapinzani wautaja uchaguzi kuwa usimikaji
- Huduma za intaneti zavurugwa Tanzania
- Rais Samia awarai Watanzania kujitokeza kupiga kura
Watanzania waamriwa kubakia nyumbani kufuatia ghasia zinazoendelea
Mitaa ya mji mkuu wa Tanzania Dar es Salaam imeipotiwa kuwa kimya mapema hii leo (30.10.2025), siku moja baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu.
Maandamano makubwa yalishuhudiwa mjini Dar es Salaam,mbeya, Arusha, Mwanza, Tunduma pamoja na miji mingine, kufuatia kutengwa kwa wagombea wa upinzani katika mchakato mzima wa uchaguzi. Ingawa matokeo bado hajaanza kutolewa rasmi, Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuendelea kushikilia nafasi yake kwa muhula mwengine wa pili madarakani.
Chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM),kimekuwepo madarakani tangu Tanzania ilipojipatia uhuru wake mwaka 1961.
Shirika la habari la AFP lilinukuu chanzo cha kidiplomasia kilichosema kuwa maandamano yaliendelea hadi usiku licha ya amri ya kutotoka nje iliyotangazwa na serikali.
Mkuu wa Polisi, IGP Camillus Wambura, alitangaza hatua hiyo kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), akisema jeshi la polisi na wanajeshi watakuwa wakifanya doria kuhakikisha amani inarejea.
Maandamano yalianza asubuhi katika maeneo ya Kimara na Ubungo, ambapo waandamanaji walichoma basi na kituo cha mafuta, huku machafuko yakiripotiwa pia Magomeni, Kinondoni na Tandale. Vyombo vya habari vya ndani viliripoti uharibifu wa vituo vya kupigia kura katika mikoa ya Arusha na Mbeya.

Dar es Salaam yatiwa kifungo kufuatia machafuko ya uchaguzi
Jeshi la polisi nchini Tanzania limetangaza amri ya kutotoka nje kuanzia saa 12 jioni Jumatano katika jiji la Dar es Salaam, kufuatia maandamano yaliyozuka wakati wa uchaguzi mkuu unaokosolewa kwa madai ya ukandamizaji dhidi ya upinzani.
Mkuu wa Polisi, IGP Camillus Wambura, alitangaza hatua hiyo kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), akisema jeshi la polisi na wanajeshi watakuwa wakifanya doria kuhakikisha amani inarejea.
Maandamano yalianza asubuhi katika maeneo ya Kimara na Ubungo, ambapo waandamanaji walichoma basi na kituo cha mafuta, huku machafuko yakiripotiwa pia Magomeni, Kinondoni na Tandale. Vyombo vya habari vya ndani viliripoti uharibifu wa vituo vya kupigia kura katika mikoa ya Arusha na Mbeya.
Hali hiyo imeibuka wakati Rais Samia Suluhu Hassan na chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwania muhula wa pili madarakani, huku wakosoaji wakilalamikia kuzuiwa kwa wagombea wa upinzani na madai ya kubanwa kwa haki za kisiasa.
Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhari ya kiusalama ukieleza kuwepo kwa maandamano katika maeneo mbalimbali nchini, huku ripoti zikionyesha uwepo wa jeshi katika Dodoma na Zanzibar, hususan karibu na ofisi za vyombo vya habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema vyombo vya ulinzi na usalama viko tayari kukabiliana na “wahalifu wa amani,” akitoa wito kwa wananchi kufuata maagizo ya serikali na kuepuka mikusanyiko isiyo halali.
Ghasia zatanda Dar es Salaam wakati uchaguzi ukiendelea
Machafuko yamezuka leo Jumatano katika jiji kuu la Dar es Salaam wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kumpa ushindi Rais Samia Suluhu Hassan, kufuatia kuondolewa kwa wagombea wakuu wa upinzani.
Mashirika ya uchunguzi wa mtandao, ikiwemo NetBlocks, yameripoti kukatika kwa huduma za intaneti kote nchini, huku video zisizothibitishwa zikionyesha vijana wakirusha mawe dhidi ya vikosi vya usalama na kituo cha mafuta kikiteketea kwa moto.
Mashuhuda wamesema mamia ya waandamanaji walielekea Daraja la Selander wakipinga mchakato wa uchaguzi, huku ripoti zikithibitisha maandamano yenye vurugu katika takribani mitaa minne ya jiji hilo.

Picha za BBC Swahili zimeonyesha polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji, ingawa serikali na jeshi la polisi bado hawajatoa kauli rasmi.
Uchaguzi huu umefanyika bila ushiriki wa chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, baada ya kiongozi wake Tundu Lissu kushtakiwa kwa makosa ya uhaini, na mgombea wa chama kingine cha ACT-Wazalendo pia akiondolewa kwenye kinyang’anyiro.
Hali hiyo imeacha wagombea wa vyama vidogo pekee wakimkabili Rais Samia, huku wachambuzi wakionya kuwa ghasia na ukosefu wa ushindani vinaweza kudhoofisha uhalali wa matokeo ya uchaguzi.
Wapinzani wauita uchaguzi kuwa “usimikaji”
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA,kimelaani uchaguzi mkuu unaoendelea, kikidai haukidhi vigezo vya kidemokrasia na kuutaja kama “taji” badala ya uchaguzi. Deogratius Munishi, katibu wa masuala ya nje wa chama hicho, ameiambia Citizen Television ya Kenya kuwa mchakato huo hauna ushindani wa kweli.
Serikali imekanusha madai hayo, ikisisitiza kuwa uchaguzi unafanyika kwa haki na uwazi, na ikapinga tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na utekaji wa viongozi wa upinzani katika kipindi cha kampeni.
Wapiga kura pia wanachagua wabunge wa Bunge la Taifa lenye viti 400 pamoja na rais na wabunge wa Zanzibar. Hata hivyo, mwitikio wa wapiga kura umeonekana kuwa mdogo katika vituo mbalimbali, huku upigaji kura ukipangwa kumalizika saa 10 jioni.
Rais Samia Suluhu Hassan, aliyepiga kura mjini Dodoma, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi wanaowataka.
Akiwa kwenye kampeni, Rais Samia amesisitiza mafanikio ya serikali yake katika kuboresha miundombinu ya usafiri na kuongeza uzalishaji wa umeme, akiahidi kuendelea kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa ndani ya siku tatu.
Intaneti yavurugwa Tanzania wakati CCM ikitafuta kurefusha utawala wake
Huduma za intaneti nchini Tanzania zilikumbwa na hitilafu kubwa Jumatano wakati mamilioni ya wananchi wakipiga kura katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo. Kundi la utetezi wa upatikanaji wa mtandao, NetBlocks, lilithibitisha kukatika kwa mtandao kote nchini, muda mfupi baada ya watumiaji kulalamikia kasi ndogo ya intaneti.
Rais Samia Suluhu Hassan, anayewania muhula wa pili kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaongoza uchaguzi uliozingirwa na wasiwasi kutoka kwa makundi ya haki za binadamu na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani. CCM imekuwa madarakani tangu Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961.
Waandishi wa habari wa Associated Press waliripoti mistari mirefu katika vituo vya kupigia kura, ambapo upigaji kura ulianza saa 1:00 asubuhi na ulipangwa kumalizika saa 10:00 jioni. Matokeo ya awali yanatarajiwa ndani ya saa 24, ingawa tume ya uchaguzi ina hadi siku saba kutangaza matokeo rasmi.

Mtandao wa intaneti unapatikana kwa tabu nchini Tanzania baada ya kuzuka matukio ya vurugu wakati wa uchaguzi.Picha: Revierfoto/IMAGO
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Tundu Lissu wa CHADEMA, bado yuko gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini baada ya kutaka mageuzi ya uchaguzi. Wakati huohuo, mgombea wa chama kingine kikubwa cha upinzani alizuiwa kushiriki. Shirika la Amnesty International lilisema uchaguzi umezingirwa na “hali ya woga,” likiripoti visa vya watu kupotezwa kwa nguvu, kukamatwa kiholela na mauaji yasiyo ya kisheria.
Rais Samia anawania muhula wake wa kwanza kamili baada ya kumalizia kipindi cha mtangulizi wake, Hayati John Pombe Magufuli, aliyefariki dunia mwaka 2021. Wagombea 16 kutoka vyama vidogo pia wanashiriki, ingawa wachambuzi wanaonya kuhusu mwitikio mdogo wa wapiga kura kutokana na imani kwamba CCM itashinda kwa urahisi.
Katika mji wa Dar es Salaam, polisi walitawanya waandamanaji waliokuwa wameitikia wito wa CHADEMA wa kufanya maandamano. Nchini Zanzibar, chama cha ACT Wazalendo kilidai dosari katika upigaji kura wa mapema, zikiwemo madai ya watu kujifanya maafisa wa usalama na kuzuia wawakilishi wa vyama, madai ambayo tume ya uchaguzi imeyakanusha ikisema uchaguzi ulifuata taratibu za kisheria.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.