Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Tume ya uchaguzi Tanzania inaendelea na zoezi la kutangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, licha ya maandamano makubwa ya umma yaliyoshuhudia ikiwemo kuchomwa kwa baadhi ya vituo vya kupigia kura.
Tume ya Uchaguzi Nchini Tanzania INEC, yasema matokeo ya awali yanammpa Samia ushindi wa zaidi ya asilimia 94 dhidi ya wagombea 16 anaochuana nao. Picha: Picture Alliance/Reuters
Unachohitaji kujua
- Matokeo ya awali yaendelea kutolewa Tanzania, Samia aongoza
- Wabunge wa Ulaya wasema uchaguzi Tanzania haukuwa wa huru na haki
- Waandamanaji wajadili mbinu za maandamano zaidi Tanzania
- Watanzania waamriwa kubakia nyumbani kufuatia ghasia zinaziendelea
- Polisi yatangaza amri ya kutotoka nje Dar es Salaam
Uchaguzi Tanzania: Samia aongoza kwa zaidi ya asilimia 94 ya kura
Uchaguzi Tanzania: Samia aongoza kwa zaidi ya asilimia 94 ya kura
Mgombea wa Urais wa chama cha mapinduzi CCM nchini Tanzania,Samia Suluhu Hassan, anaongoza kwa zaidi ya asilimia 94 ya kura zilizopigwa kwa nafasi ya urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Nchini Tanzania INEC, Jaji Jacob Mwambegele, matokeo ya awali katika majimbo 19 ambayo kura zake zimekwisha hesabiwa hadi sasa, yanammpa Samia ushindi wa zaidi ya asilimia 94 dhidi ya wagombea 16 anaochuana nao.
Jaji Mwambegele: Kura katika majimbo 19 tayari zimeshahesabiwa
Tume huru ya uchaguzi iilisema itatangaza mshindi wa nafasi ya urais ndani ya saa 72 baada ya kukamilika zoezi la kupiga kura. Uchaguzi wa Tanzania mwaka huu umefanyika bila kuwepo wapinzani wenye nguvu.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania INEC Jaji Jacob Mwambegele, akitangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Oktoba 29.Picha: INEC Tanzania
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA Tundu Lissu, anaendelea kuzuiliwa jela kwa makosa ya uhaini, baada ya kudai marekebisho ya mifumo ya uchaguzi. Mgombea wa Urasi wa chama cha pili kwa ukubwa cha upinzani nchini Tanzania ACT Wazalendo, Luhaga Mpina alinyimwa nafasi ya kushiriki uchaguzi huo.
Uchaguzi wenyewe umekumbwa na matukio ya uvunjifu wa amani katika baadhi ya maeneo hususan miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Tunduma na Mbeya. Mitandao ya inteneti pia ilivurugwa huku kukiwa na ripoti za mauaji ya watu kadhaa hii ikiwa ni kulingana na shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International.
Wabunge wa Ulaya wasema uchaguzi Tanzania haukuwa wa huru na haki
Idadi ya waliojitokeza wakati wa uchaguzi wa Jumatano Oktoba 29, ilikuwa ndogo, na machafuko yalizuka baadae mchana, wakati waandamanaji walipoanza kuchoma moto basi, kituo cha mafuta, kushambulia vituo vya polisi na kuharibu vituo vya kupigia kura pamoja na mali za umma.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International, limesema katika vurugu hizo watu wawiili wameuwawa akiwemo raia wa kawaida na afisa mmoja wa polisi.

Amnesty International yatoa wito wa uchunguzi kufanyika kuhusu madai ya polisi Tanzania kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.Picha: AP Photo/picture alliance
Serikali bado haijathibitisha wala kutoa maoni yoyote juu ya vifo hivyo. Amnesty International pia imetoa wito wa kufanyika uchunguzi, kuhusu madai ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.
Huduma za usafiri wa majini zasimamishwa kwa muda
Kwengineko huduma za usafiri wa majini, kutokea Tanzania bara kuelekea visiwani Zanzibar, imesimamishwa kwa muda katika eneo hilo ambako matokeo yake ya uchaguzi huenda yakatangazwa leo Alhamisi (30.10.2025)
Watanzania walishiriki Uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba, 2025, kumchagua rais, wabunge na madiwani. Kiongozi Mkuu wa upinzani ambae pia ni mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA Tundu Lissu, anaendelea kuzuiliwa jela kwa makosa ya uhaini, baada ya kudai marekebisho ya mifumo ya uchaguzi.
Mgombea wa Urasi wa chama cha pili kwa ukubwa cha upinzani nchini humo ACT Wazalendo, Luhaga Mpina alinyimwa nafasi ya kushiriki uchaguzi huo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.