Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Polisi katika mji wa Dar nchini Tanzania wamefyatua risasi na vitoa machozi siku ya Alhamisi kutawanya waandamanaji waliorejea barabarani siku moja baada ya uchaguzi.
Raia wa Uingereza walioko Tanzania watakiwa kuchukua tahadhari
Raia wa Uingereza wanaoishi nchini Tanzania wameshauriwa kuchukua tahadhari na kujilinda kufuatia ghasia na maandamano yanayoendelea kuripotiwa nchini humo.
Kulingana na taarifa ya ubalozi wa Uingereza iliotolewa tarehe 30 Oktoba, ubalozi huo aidha umewashauri raia wake wafuate amri zinazotolewa na serikali ya Tanzania kipindi hiki.
‘Zingatieni amri ya kutotoka nje, fuata ushauri wa serikali za mitaa na pia epukeni maandamano’, yasema taarifa hiyo.
Vurugu za uchaguzi Tanzania: Hali ikoje Mwanza?
Hali ya sintofahamu iliendelea kushuhudiwa mjini Mwanza usiku wa kuamkia leo kutokana na hali ngumu iliyotokana na maandamano ya vijana maarufu Gen Z wakipita katika maeneo mbali mbali ya mji na kuzua hali ya taharuki hasa walipokuwa wakipambana na vikosi vya usalama.
mali Milio ya risasi na mabomu ya machozi ilisikika katika maeneo kadha wa kadha ya jiji hilo.
Kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi kuelekea eneo la Buhongwa waandamanaji wameripotiwa kufukuzana na polisi baada ya kituo cha polisi kuteketezwa.
Katika barabara kuu kutoka Mwanza mjini kuelekea eneo la uwanja wa ndege waandamanaji walipambana na polisi wamekuwa wakipambana vilivyo na ofisi ya kata na kituo kidogo cha polisi nacho kikachomwa moto. Katika eneo la Nyamanolo mkabala na Fwatiati hali sio shwari kwani huko pia kituo cha polisi na ofisi ya kata ya CCM kilichomwa moto.
Waandamanaji pia walivamia duka kubwa la jumla yaani Super Market na kulipora.
Watumishi wa umma Tanzania kuendelea kufanya kazi nyumbani

Msemaji wa serikali Gerson Msigwa ametoa taarifa inayowataka watumishi wa umma kuendelea kufanyia kazi nyumbani isipokuwa kwa wale ambao majukumu yao ya kazi yanawahitaji kuwa katika vituo vyao vya kazi.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa ni kufuatia angalizo la kiusalama lililotangazwa jana Jumatano 29,Oktoba,2025 na Jeshi la Polisi.
Aidha wanafunzi wote wa shule na vyuo wameombwa kuendelea kujisomea manyumbani na waajiri katika sekta binafsi wameshauriwa kuzingatia tahadhari hiyo na kuwaruhusu wafanyakazi wao kufanyia pia kazi majumbani.
Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania Camillius Wambura jana alitangaza amri ya kutotoka nje mjini Dar es Salam kuanzia saa kumi na mbili jioni.
Hatua hizo zinafuatia maandamano ya umma yaliyoshuhudiwa katika miji mbali mbali nchini Tanzania,kupinga uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano 29,Oktoba, 2025.
Maandamano yaripotiwa Namanga upande wa Tanzania

Maandamano yananaendelea kwa sasa katika mji wa mpakani wa Namanga upade wa Tanzania.
Kwa mujibu wa mashuhuda raia wa Kenya wameungana na majirani zao kwenye maandamano baada ya mtu mmoja kudaiwa kuuawa kwenye purukushani hizo.
Milio ya risasi na mabobu ya machozi yanarushwa kutoka pando zote mbili za mpaka wa Namanga wa Kenya na Tanzania.
Awali moshi ulionekani ukifuka upande wa mpaka wa Tanzania.
Shughuli za kibiashara zimekwama huku hali ya taharuki ikizidi kuongezeka.
Malori ya kusafirisha bidhaa kutoka na kuingia nchini humo yamekwamba mpakani.
Marekani yatoa tahadhari ya kiusalama kwa raia wake wanaoishi Tanzania
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari ya kiusalama kwa raia wa taifa hilo wanaoishi nchini humo .
Kulingana na tahadhari hiyo ubalozi huo umewataka raia wa taifa hilo kuepuka maandamano yanayoendelea, kuepekuka mikusanyiko ya watu kufuatialia kwa karibu taarifa za vyombo vya habari ili kujifahamisha yanayoendelea mbali na kuchukua tahadhari ya juu katika maeneo waliopo.
Hatua hiyo inajiri kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo.
Kulingana na taarifa hiyo kuna ripoti za maandamano kote nchini ambayo yamesababisha kuzuka kwa ghasia na kufungwa kwa baadhi ya barabara.
Ripoti hiyo imeelezea kwamba baadhi ya barabara kama ile ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere imefungwa.
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuhusu kuzimwa kwa mtandaohali ambayo imeathiri pakubwa mawasiliano.
Uchaguzi Tanzania 2025: Tume ya Uchaguzi Tanzania yaanza kutangaza matokeo

Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania INEC imeanza kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais.
Hadi kufikia sasa ni mikoa minne pekee iliofanikiwa kuwasilisha matokeo yake.
Kulingana na matokeo hayo Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama tawala cha CCM Samia Suluhu Hassan anaongoza kulingana na kura zilizohesabiwa.
Aidha maandamano yameripotiwa katika eneo la Meriwa lililopo barabara ya jiji kuu la Dodoma na Dar es Salaam ambapo polisi wamewatawanya waandamanaji.
Polisi vilevile wameripotiwa kufunga barabara ya Singida – Arusha kwa hofu ya kuzuka maandamano zaidi.
Maandamano yaendelea kwa siku ya pili mjini Dar es Salaam

Polisi katika mji wa Dar nchini Tanzania wamefyatua risasi na vitoa machozi siku ya Alhamisi kutawanya waandamanaji waliorejea barabarani siku moja baada ya uchaguzi uliogubikwa na maandamano yenye vurugu, kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters.
Maandamano yalizuka mjini Dar es Salaam na miji mingine kadhaa wakati wa upigaji kura siku ya Jumatano, huku waandamanaji wakilalamikia kukamatwa kwa viongozi wakuu wa upinzani na kuzuiliwa kushiriki katika uchaguzi wa Urais mbali na madai ya ukandamizaji wa wakosoaji wa serikali.
Kwa mujibu wa Reuters baadhi ya maeneo ambayo maandamano hayo yameripotiwa kufanyika hii leo ni pamoja na Mbagala, Gongo la Mboto and Kiluvya.
Hali ya wasiwasi yaendelea kuripotiwa Tanzania

Hali ya wasiwasi inaendelea kushuhudiwa nchini Tanzania kufuatia maandamano ya ghasia yaliofanyika hapo jana.
Hatahivyo baadhi ya barabara ambazo zilikuwa zimefungwa hapo jana sasa zimefunguliwa.
Baadhi ya raia ambao walikuwa wamekwama kutokana na maandamano yaliosababisha amri ya kutotoka nje kuwekwa hapo jana wamefanikiwa kufika makwao.
Aidha kuna ripoti za maandamano kuzuka katika mji wa kaskazini wa Mwanza.
Taarifa mjini humo zinasema kwamba waandamanaji walifanikiwa kupenya hadi katikati ya jiji na kusababisha makabiliano ya umwagaji damu dhidi ya polisi.
Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa kwa idadi ya watu na biashara baada ya Dar Es Salaam na liko kwenye mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria.
Aidha kuna madai kwamba baadhi ya waandamanaji mjini Dar, Mbeya na Dodoma wamekuwa wakiwashambulia walioshiriki katika shughuli ya kupiga kura hapo jana
Vilevile huku mitandao ikiendelea kuminywa kwa siku ya pili mfululizo ni simu za kawaida pekee zinazotumika kwa mawasiliano.
Kiongozi wa RSF Sudan aahidi uchunguzi huku ghadhabu ikiongezeka kufuatia mauaji ya el-Fasher

Kiongozi wa kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti, ameahidi kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ukiukaji wa haki uliofanywa na askari wake wakati wa oparesheni ya kuuteka mji wa el-Fasher, Darfur.
Tangazo hilo linakuja baada ya kuongezeka kwa ripoti za mauaji ya raia wengi kufuatia RSF kuchukua udhibiti wa mji huo siku ya Jumapili, hatua iliyozua hasira kali katika jumuiya ya kimataifa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuitisha kikao maalum kujadili hali ya Sudan, ambayo sasa imo katika mwaka wa tatu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF.
Kupitia taarifa yake, Hemedti alieleza masikitiko yake kwa “janga lililowakumba watu wa el-Fasher,” na akakiri kwamba “kulikuwepo ukiukaji” uliofanywa na baadhi ya wanajeshi wake.
Aliongeza kuwa kamati maalum imeundwa na tayari imewasili mjini humo kufanya uchunguzi wa kina.
Hata hivyo, wachambuzi wamesalia na mashaka, wakikumbusha kuwa ahadi kama hizo ziliwahi kutolewa mara kadhaa ikiwemo baada ya tuhuma za mauaji ya halaiki mjini el-Geneina mwaka 2023, na ukatili uliofanywa wakati wa udhibiti wa RSF katika jimbo la kati la Gezira bila kuchukuliwa hatua zozote za kweli.
Tukio la el-Fasher limezidisha hofu kwamba machafuko ya Darfur yanaweza kuingia katika awamu mpya ya ukatili, huku dunia ikitoa wito kwa pande zote kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu.
Rais Trump apunguza ushuru kwa China baada ya kukutana na rais Xi

Mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na China yameelezwa kuwa “hatua chanya isiyoweza kupuuzwa kuelekea utulivu wa muda katika uhusiano wenye mvutano,” amesema Louise Loo wa Oxford Economics.
Hata hivyo, masuala makuu manne yakiwa ni hali ya Taiwan, usafirishaji wa bidhaa kupitia nchi za kati, TikTok na Teknolojia bado hayajatatuliwa.
“Hatua ya leo imefungua njia ya ushirikiano wa kina kuelekea 2026,” alisema Loo, akionya pia kuwa “hatari ya makosa ya kisera na tafsiri potofu bado ni kubwa.”
Makubaliano ya kulegeza udhibiti wa mauzo ya nje ya madini adimu yanatarajiwa kutoa nafuu ya muda mfupi kwa Marekani.
Serikali ya Trump imewekeza katika mgodi wa Mountain Pass nchini California na inatafuta vyanzo vingine kutoka kwa Greenland, Brazili na Australia.
Hata hivyo, suala la TikTok halikupata suluhisho.
Taarifa ya China ilisema: “China itashirikiana na Marekani kutatua ipasavyo masuala yanayohusiana na TikTok.”
Ikulu ya White House inataka kitengo cha Marekani kijitenge na kampuni mama ya China ByteDance, kwa sababu za usalama wa taifa, huku Waziri wa Fedha Scott Bessent akisema makubaliano yako tayari “kukamilishwa Alhamisi.”
Trump alisaini amri ya kuruhusu TikTok iendelee kuendeshwa chini ya umiliki wa Wamarekani, lakini mkutano wa leo haukutoa makubaliano mapya.
Wanaume wawili wahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa kula njama na Iran ya kumuua mpinzani wake

Wanaume wawili waliopatikana na hatia ya makosa ya mauaji walihukumiwa huko New York kila mmoja kifungo cha miaka 25 jela kwa kile waendesha mashtaka walichokiita njama iliyofeli iliyoungwa mkono na Iran ya kumuua mpinzani wa Iran anayeishi Marekani.
Rafat Amirov, 46, na Polad Omarov, 41, walifika katika mavazi ya jela mbele ya Jaji wa Wilaya ya Marekani Colleen McMahon huko Manhattan.
Mahakama iliwapata na hatia mwezi Machi kwa mashtaka matano – ikiwa ni pamoja na kujaribu kuua, kutakatisha fedha na kula njama – kwa majukumu yao katika njama ya 2022 ya kumuua Masih Alinejad, Mmarekani mwenye asili ya Iran na mkosoaji mkubwa wa Tehran na jinsi inavyowatendea wanawake.
“Huu ulikuwa uhalifu mbaya ambao umekuwa na athari mbaya kwa watu wengine wazuri,” McMahon alisema.
Alinejad alihutubia mahakama huku umati wa wafuasi wake wakiwa wameketi nyuma yake, wakisema Amirov na Omarov walibadilisha maisha yake juu chini lakini walishindwa kummaliza.
“Nilivuka bahari kuja Marekani ili kuwa na maisha ya kawaida, lakini sina,” Alinejad alisema, huku watu wakimpigia makofi alipokuwa akitoka kwenye jukwaa.
Adhabu hizo zilitolewa chini ya miaka 55 kwa kila mwanamume anayetafutwa na waendesha mashtaka na zaidi ya miaka 10 hadi 13 iliyopendekezwa na upande wa utetezi.
Mawakili wa Amirov na Omarov walihimiza jaji kuwa na huruma, wakitaka kuonyesha jinsi uhusiano wa mteja wao na Tehran usivyo muhimu na majukumu katika njama hiyo.
Hawakujibu mara moja barua pepe za kutaka maoni yao Jumatano
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.