Israel yafanya uvamizi kusini mwa Lebanon

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Wanajeshi wa Lebanon katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na IsraelPicha: Karamallah Daher/REUTERS

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa limefanya uvamizi kusini mwa Lebanon. Duru za habari ziliripoti kuwa vikosi vya Israel vilivamia jengo la manispaa na kumuuwa mwajiriwa Ibrahim Salameh akiwa amelala.

Israel kwa upande wake imebainisha kuwa mashambulizi hayo ya usiku wa kuamkia Alhamisi yalikuwa operesheni dhidi ya miundombinu ya kundi la Hezbollah na Salameh alikuwa mtuhumiwa.

Rais wa Syria aamuru jeshi kukabiliana na uvamizi wowote

Wanakijiji walioshuhudia tukio hilo wamesema uvamizi wa Israel ulidumu kwa saa kadhaa na kuwa wanajeshi waliondoka mapema alfajiri. Kufuatia mashambulizi hayo Rais wa Lebanon Joseph Aoun ameliamuru jeshi  kukabiliana na vitendo vya aina hiyo ili kulinda mipaka na wananchi wake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment