WFP yathibitisha kufukuzwa kwa maafisa wake wakuu Sudan

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Msaada wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani- WFP nchini SudanPicha: Mahamat Ramadane/Reuters

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limethibitisha kufukuzwa kwa wafanyakazi wake wawili wakuu nchini Sudan.

Katika taarifa, shirika hilo lenye makao yake mjini Rome, Italia, limesema mkurugenzi na mratibu wa shirika hilo nchini Sudan wameorodheshwa kuwa watu wasiostahili kuwa nchini humo na kutakiwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 72 bila ya maelezo yoyote.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa maafisa wake na wengine wakuu wa Umoja wa Mataifa wanawasiliana na mamlaka ya Sudan kupinga uamuzi huo, ambao wanasema umekuja katika wakati muhimu kwa nchi hiyo.

Sudan inahitaji msaada mkubwa wa kibinadamu

Taarifa ya WFP imesema hitaji la msaada wa kibinadamu nchini humo ni la juu zaidi huku zaidi ya watu milioni 24 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na jamii kuathiriwa na njaa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika wakati ambapo WFP na washirika wake wanahitaji kupanua ufikiaji wao wa watu, maamuzi hayo yanalilazimu kufanya mabadiliko ya ghafla ya uongozi na kutatiza shughuli zake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment