Watu 64 wauawa katika ghasia za mjini Rio de Janeiro

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Operesheni ya polisi dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya Rio de JaneiroPicha: Jose Lucena/TheNEWS2/ZUMA/picture alliance

Watu 64 wameuawa katika makabiliano ya mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, baada ya polisi kuanzisha msako mkubwa zaidi kuwahi kutokea dhidi ya magenge ya dawa za kulevya.

Watu 64 wameuawa katika makabiliano ya mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, baada ya polisi kuanzisha msako mkubwa zaidi kuwahi kutokea dhidi ya magenge ya dawa za kulevya.

Takriban maafisa 2,500 waliokuwa na silaha nzito, wakisaidiwa na magari ya kivita, helikopta na ndege zisizo na rubani walishiriki katika operesheni hiyo, iliyolilenga genge kuu la ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Brazil katika vitongoji viwili maskini, kaskazini mwa Rio.

Milio ya risasi ilisikika katika maeneo ya karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege huku moshi mzito ukifuka kutokana na milipuko kadhaa.

Wakaazi walihangaika kutafuta mahali pa kujificha na maduka yakifunga milango yake. Serikali kuu ya Brazil imesema msako huo ulilenga kukomesha genge moja linaloitwa Comando Vermelho.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment