Usiogope kuchukua hatua..

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

HADI SASA…

Hadi sasa unaogopa kuchekwa?

Hadi sasa bado unatoa visingizio badala ya kuchukua hatua?

Hadi sasa unalaumu wazazi kwamba hawajakupatia mtaji?

Hadi sasa bado unalalamika hawakukusomesha?

Hadi sasa huoni fursa zilizoko kila kona?

Hadi sasa unasubiri hali iwe nzuri ndipo uanze?

POLE SANA…

Maana kila dakika unayosubiri, dunia inaendelea kusonga.

Wale unaowaona wakifanikiwa si kwamba wana bahati zaidi, la hasha.?

Ni kwamba waliamua kufanya, hata pasipo kuwa na hali kamili.Waliamua kujaribu, wakashindwa, lakini hawakukata tamaa.

Waliamua kusimama tena, na leo wanavuna matunda ya juhudi zao.

Na wewe bado unasubiri “wakati muafaka”?

Ukweli ni huu hakuna wakati muafaka,

isipokuwa ule utakapoamua KUANZA SASA.

ANGALIA VIZURI…

Fursa ziko kila mahali..mitandaoni, mitaani, kwenye ujuzi mdogo ulionao, katika kipaji ulichopewa na Mungu, kwenye wazo ulilolipuuza jana.

Lakini fursa hizo hazitakufuata,

zinamsubiri yule mwenye ujasiri wa KUCHUKUA HATUA.

DECEMBER imekaribia…

Na bado haujafanya kitu kikubwa kwa mwaka huu.

Je, utaruhusu mwaka uishe ukiwa na maneno yale yale ya “nitafanya”?

Utaendelea kuahirisha maisha yako hadi lini?

MWAKA HAUKUSUBIRI.

Watu wanapiga hatua, wengine wanaanza biashara ndogo,wanasoma, wanajifunza, wanajenga chapa zao, wanajenga ndoto za na wewe bado unawaza “mambo yakikaa sawa nitafanya”?

AMKA LEO.

Usisubiri hali iwe bora … anza na ulicho nacho.

Usiogope kushindwa …kushindwa ni sehemu ya safari.

Usiogope kuchekwa …wale wanaocheka leo,

kesho watakuuliza uliwezaje kufika hapo ulipo.

Usiishi ukilaumu wazazi, serikali, au mazingira. Maamuzi yako leo ndiyo yataamua kesho yako.

Mabadiliko yako hayataanza hadi utakapochukua hatua.

Mafanikio hayawezi kufikiwa kwa maneno,

bali kwa vitendo, bidii, na uthubutu.

Hata hatua ndogo leo ni bora kuliko mipango mikubwa isiyotekelezwa.

Usikubali mwaka uishe bila kufanya kitu kikubwa.

Chukua hatua leo.

Andika, anzisha, jaribu, jifunze, au rekebisha.

Haijalishi wapi upo — muhimu ni kuanza.

MUDA HAUTAKUSUBIRI.

Vuka visingizio vya kutokufanya.

Simama, chukua hatua, na amini unaweza.

Nakutakia ushindi mkubwa, uthubutu mkubwa.

NINI NI KIZUIZI KWAKO.?

Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment