Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Bango la Rais Samia Suluhu HassanPicha: AP Photo/dpa/picture alliance
Watanzania wanapiga kura leo katika uchaguzi mkuu ambao Rais Samia Suluhu Hassan anachuana na wagombea kutoka vyama vidogo.
Watanzania wanapiga kura leokatika uchaguzi mkuu ambao Rais Samia Suluhu Hassan anachuana na wagombea kutoka vyama vidogo. Wapiga kura watamchagua rais, wabunge, madiwani na wawakilishi.
Uchaguzi wa leo unafanyika bila ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA, ambacho mwenyekiti wake Tundu Lissu anakabiliwa na mashtaka ya uhaini ambayo ameyakana.
Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania INEC ilikiengua chama hicho baada ya kukataa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi mapema mwaka huu.
Tume hiyo pia ilimuengua mgombea wa chama kingine cha upinzani cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina baada ya pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuwaacha wagombea wa vyama vidogo pekee kuchuana na Rais Samia.
Tume ya uchaguzi inasema kuwa itatangaza matokeo rasmi ndani ya siku tatu kutoka siku ya uchaguzi. Mashirika haki za binadamu ikiwemo Amnesty International yameshutumu mamlaka za Tanzania kwa kukandamiza upinzani, madai ambayo serikali ilikanusha.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.