Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Waziri wa ulinzi wa Pakistan Khawaja Mohammad Asif, ameionya Afghanistan kuwa shambulio lolote la kigaidi au la kujitoa mhanga kufa litakalofanywa na wanamgambo nchini Pakistan litasababisha jibu kali la kisasi.
Afghanistan haijatoa tamko juu ya kutibuka kwa mazungumzo kati yake na Pakistan ama pia kuhusu matamshi ya Asif, lakini shirika la utangazaji la serikali ya Afghanistan, RTA, limeripoti kuwa mazungumzo yalikwama kwa sababu ya kile ilichokiita “matakwa yasiyo na mantiki” kutoka Pakistan.
Afghanistan yasema Tehrik-e-Taliban Pakistan ni suala la ndani la Pakistan
Kulingana na RTA, Pakistan ilitaka hakikisho kwamba hakuna mashambulizi yatakayotokea kutoka Afghanistan, huku ujumbe wa Taliban ukisema kundi la Taliban la Pakistan, almaarufu Tehrik-e-Taliban Pakistan, ni suala la ndani la Pakistan.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.