Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: Julien Mattia/Le Pictorium/MAXPPP/picture alliance
Ukraine imesema leo kuwa maafisa wake wa usalama wanamshikilia mkufunzi mmoja wa zamani wa jeshi kutoka nchi ya Ulaya ambayo haikutajwa jina kwa shtuma za kuifanyia Urusi ujasusi dhidi ya jeshi la Ukraine.
Katika taarifa, Huduma ya Usalama ya Ukraine (SBU) imesema kulingana na nyenzo za kesi hiyo, raia huyo wa kigeni alitoa taarifa rasmi kwa kile ilichokieleza kuwa adui kuhusu vikosi vya ulinzi vya Ukraine na alikuwa akijiandaa kufanya vitendo vya kigaidi.
Mshukiwa atoa adaiwa kutoa maelezo ya usalama kwa Urusi
Taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu mshukiwa huyo lakini imesema alitoa maelezo kwa Urusi kuhusu wakufunzi wengine wa kijeshi wa kigeni wanaofanya kazi nchini Ukraine pamoja na waratibu wa vituo vya mafunzo vya jeshi.
Taarifa hiyo ya SBU imeendelea kusema kuwa huduma ya usalama na ujasusi ya Urusi FSB, ilitoa maagizo kwa mtu huyo ya kutengeneza vifaa vya vilipuzi na pia kumpa bunduki na risasi.
Mshukiwa huyo amezuiliwa katika makazi yake mjini Kyiv.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.