Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Ukipata FAIDA Kwenye biashara yako ni muhimu sana kuzingatia mambo haya muhimu na kuyaepuka…
…
1. Kutumia faida yote kwa anasa
Badala ya kuwekeza tena kwenye biashara, wengine huanza kununua vitu visivyo vya lazima simu mpya, nguo, au starehe.
Kumbuka: Faida ya kwanza ni damu ya biashara, si pesa ya matumizi.
…
2. Kutotenga kati ya fedha za biashara na za binafsi.
Wengi huchanganya pesa ya biashara na matumizi ya nyumbani.
SULUHISHO LAKE.Fungua akaunti tofauti ya biashara, hata kama ni ndogo.
…
3. Kutofanya hesabu sahihi ya faida
Wengine hudhani wametengeneza faida, kumbe hawajakata gharama zote.
KUMBUKA KUWA Faida halisi ni baada ya kutoa gharama zote, usafiri, kodi, malighafi, n.k.
…
4. Kutokuweka akiba au dharura.
Biashara ina misimu leo faida, kesho hasara.
Ukishindwa kuweka akiba huwezi kufanikiwa KIFEDHA.
UNAHITAJI KUWEKA akiba ili biashara isitetemeke unapopata changamoto.
…
5. Kutokuwekeza tena kwenye biashara
Faida inapaswa kurudi kwenye biashara ili ikue… ongeza bidhaa, boresha huduma, au tangaza zaidi.
UNAHITAJI..Kuwekeza ili biashara ijitanue.
…
6. Kujisifu mapema au kuonyesha mafanikio kabla hayajakaa
Wengine hutumia faida ya kwanza kujionyesha mitandaoni au kujisifia na kusahau kujenga msingi.
Kimya kinajenga, makelele yanaharibu.
…
7. Kushindwa kujifunza zaidi
Wengi wakishapata faida kidogo hujisikia wamefanikiwa sana.
Endelea kujifunza kuhusu fedha, masoko, na uongozi biashara inahitaji ubongo kuliko nguvu.
Ni jambo gani ambalo bado unahitaji usimamizi kati ya haya?
Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.