Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Mwili wa mateka wa Israel wapatikana kutoka kwenye handakiPicha: Abdallah F.s. Alattar/Anadolu/picture alliance
Shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema kwamba Israel imefanya mashambulizi ya anga siku ya Jumanne licha ya makubaliano ya usitishaji mapigano yanayoendelea.
Shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema kwamba Israel imefanya mashambulizi ya anga siku ya Jumanne licha ya makubaliano ya usitishaji mapigano yanayoendelea, baada ya jeshi la Israel kuishutumu Hamas kwa kushambulia wanajeshi wake na kukiuka makubaliano.
Takriban watu 30 wameuawa katika mashambulizi yaliyolenga maeneo kadhaa ya Gaza, alisema msemaji wa shirika hilo, ambalo linafanya kazi kama kikosi cha uokoaji chini ya Hamas.
Hata hivyo makamu wa rais wa Marekani JD Vance alidai kuwa makubaliano hayo bado yanadumu licha ya mapigano ya jumanne. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu aliamuru mashambulizi makali huko Gaza, huku Waziri wa Ulinzi Israel Katz akiishutumu Hamas kwa kushambulia wanajeshi wa Israel huko huko Gaza.
Hapo jana Israel ilidai kuwauwa wanamgambo watatu wa Kipalestina wakati wa operesheni kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.