Idadi ndogo ya wapiga kura yashuhudiwa nchini Tanzania

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Zoezi la kupia kura mjini Stone Town, ZanzibarPicha: Marco Longari/AFP

Idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza katika jiji kuu la Tanzania, Dar es Salaam, leo kwa zoezi la uchaguzi huku wapinzani wakuu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa aidha wamefungwa jela ama kuzuiwa kugombea.

Vituo vya kupiga kura katika baadhi ya maeneo yenye shughuli nyingi zaidi jijini humo vilikuwa tupu saa moja baada ya kufunguliwa, licha ya kuwa na shughuli nyingi wakati kama huo wakati wa chaguzi zilizopita.

Haya yameripotiwa na shirika la habari la AFP.

Watu kuhamasishwa kupiga kura

Afisa mmoja kutoka chama tawala, Chama cha Mapinduzi, CCM wilayani Temeke  Dar es Salaam, aliyezungumza na AFP kwa sharti la kutotajwa jina, amesema watawahamasisha watu mitaani na majumbani kutoka na kupiga kura.

Awali shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilaani kile ilichokitaja kuwa “wimbi la ugaidi” kabla ya uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na “kutoweka na kuteswa kwa watu pamoja na mauaji ya kiholela ya viongozi wa upinzani na wanaharakati.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment