Wapiga kura visiwani Zanzibar kushiriki kura ya mapema leo

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Wapiga kura wakihakiki majina yao Kikwajuni ZanzibarPicha: Glenn Carnell/State House Zanzibar

Wapiga kura visiwani Zanzibar leo wanaanza zoezi la kupiga kura katika kile kinachofahamika kuwa ni “kura ya mapema” ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Wapiga kura visiwani Zanzibar leo wanaanza zoezi la kupiga kura katika kile kinachofahamika kuwa ni “kura ya mapema” ya uchaguzi mkuu wa Tanzania. Uchaguzi huo unafanyika siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa kesho Oktoba 29, utakaofanyika Tanzania bara na visiwani.

Rais wa sasa Hussein Mwinyi, kupitia chama tawala cha mapinduzi, CCM, anakabiliana na makamu wake wa kwanza, Othman Masoud Othman kupitia chama cha upinzani cha ACT Wazalendo. Chama hicho kimekuwa kikipinga kura hiyo ya mapema.

Vituo vya kura ya mapema vitafunguliwa saa moja asubuhi saa za Afrika Mashariki na kufungwa saa 10 jioni na matokeo ya urais yatatangazwa ndani ya saa 72 kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC.

Kampeni za uchaguzi zilizoanza Septemba 11 zilikamilika jana Oktoba 27.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment