UPO CHUO AU MAZINGIRA YA CHUO,FANYA BIASHARA HIZI 12 UTAPATA MATOKEO MAKUBWA…

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Ukiwa mwanafunzi wa chuo, Au mazingira ya chuo bado unaweza kuingiza kipato kupitia biashara ndogondogo zinazolenga mahitaji ya wanafunzi.

Hapa kuna baadhi ya biashara rahisi lakini zenye faida kubwa. Chagua yako..

1.Biashara ya Mavazi (Mitumba, Tshirts, Vitenge)

Nunua kwa bei ya jumla sokoni Kariakoo, Manzese, Karume, au hapo ulipo duka la jumla. Kisha uuze kwa wanafunzi.

Lenga bidhaa zinazopendwa kama jeans, viatu, au t-shirts zenye maandishi ya kuvutia.Tumia WhatsApp/Instagram kuuza.

2.Kupika na Kuuza Chakula au Vitafunwa

Chapati, maandazi, sambusa, keki, chipsi au juice.Unaweza kuuza kwa darasani, hostel, au kuweka canteen. Pata oda kwa wanafunzi waliobanwa na muda kisha wauzie.

3. Uuzaji wa Accessories za Kike

Cheni, pete, hereni, mitandio, nywele bandia, na rangi za kucha ni bidhaa zinazopendwa sana na wadada wa chuo.Nunua Kariakoo hasa mtaa wa Mchikichi na Sikukuu.Tumia Instagram, WhatsApp na group za darasa kutangaza.

2.Uza nguo za ndani.

Wengi hupenda kubadilisha nguo za ndani kulingana na mazingira. Unaweza kuuza nguo za kike na kiume. Biashara hii inafaida sana kwani unanunua kwa bei ndogo na unauza kwa bei nzuri.

Chimbo la chupi kariakoo ni mtaa wa mchikichi na gogo.Utapata boxer za kiume pia na nguo za ndani. Huko ukiwa na laki na nusu unapata mzigo wa kuanza biashara ndogo. ( maduka zaidi yapo kariakoo – mchikichi inapokutana na swahili)

3.Kuanzisha Online Store.

Fungua duka la mtandaoni kwa kuuza bidhaa za rafiki zako au zako.Unaweza kuuza vitu bila hata kuwa na stock (dropshipping ya ndani).

4. Uuzaji wa Phone Accessories

Uza chaja, earphones, screen protectors, line za simu, n.k.

Jifunze pia ufundi mdogo wa simu kama kubadilisha display au kuchomea chaja.Wanachuo wengi wana simu bidhaa zako zitauzika kila siku.

5.Uuzaji wa Vipodozi & Skin Care

Warembo wa chuo wanahitaji ngozi nzuri na bidhaa bora. Piga picha za bidhaa toka madukani Kariakoo (mtaa wa Jangwani & Mafia).Chukua oda online, kisha peleka mzigo kwa mteja. Jibrand kama mtu unayeweza kusaidia ngozi mbaya irudi kwenye ubora wake utaaminika haraka.

6.Mobile Money / Sajiri laini/Uwakala Mdogo.

Uwe wakala wa M-Pesa, TigoPesa au malipo ya LUKU/DSTV. Rusha vifurushi vya chuo.Wanafunzi wanahitaji huduma hizo kila siku. Unahitaji kuwa na laini za miamala mbalimbali. Na connection ya mawakala wa kuu.

7.Huduma ya Kupiga Picha,Video Editing.

Kama una kamera au simu nzuri, pigia watu picha, tengeneza content za birthdays, graduation, au poster za matangazo.Tumia skills zako kama unajua Photoshop, Canva au CapCut utapata matokeo makubwa.

8.Online Freelancing (Kazi za Mtandaoni)

Kama unajua kuandika, kutafsiri, au kutumia Excel/Word vizuri, fanya kazi kwenye tovuti kama Upwork, Fiverr au Workana.Muda kama unaruhusu, na unaweza kufanya popote.

9.Huduma ya Kuchapa, Kuandika na Kuprinti (Stationary)

Kama una laptop/printer, tengeneza pesa kwa kuchapa assignments, CVs, na project papers.Kwa mazingira ya chuo utapiga sana hela kwani vitu vingi hutegemea hili.

10.Graphic Design.

Fanya kazi za kuchora mabango, logo, kutengeneza posters, nk, katika muda wako ziad. Shughuli ni nyingi sana utapata wateja wengi.

11.Biashara za huduma (Service-based) Mfano kuwa MC,mpambaji shughuli nyingi hufanyika jioni au weekend. Kwa wewe mwanafunzi inakupa nafasi kubwa kufanya.

12.Fundisha watu/Coaching .

Kama una maarifa, fundisha wengine kwa njia ya mtandao.Kama biashara, social media management.(Usimamizi wa mitandao ya kijamii.)n.k

Ni biashara gani umeipenda zaidi.? Niandikie hapa chini kwenye comment ili tujadiliane pamoja.

Share ujumbe huu kwa wanachuo wengine ili waweze kujenga uchumi binafsi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment