Takaichi, Trump kuangamiza zana za nyuklia Korea Kaskazini

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi, amesema yeye pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump wamethibitisha kwa mara nyengine dhamira yao ya kukamilisha uangamizaji wa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini.

Takaichi amesema viongozi hao wawili wamekubaliana hayo katika mkutano wa kilele leo huko mjini Tokyo.

Takaichi na Trump vile vile wamesisitiza umuhimu wa amani Taiwan ingawa amekataa kutoa tamko lolote juu ya walichokijadili kuhusu China kwa sababu Trump atakutana na Rais wa China hivi karibuni.

Haya yanafanyika wakati ambapo mtu mmoja anayetuhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe miaka mitatu iliyopita, leo amekiri kumuua kiongozi huyo, wakati kesi dhidi yake ilipokuwa ikisikilizwa kwa mara ya kwanza.

Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 45 alikamatwa katika eneo la tukio hilo Julai 2022 baada ya kudaiwa kumfyetulia risasi Abe aliyekuwa anahutubia umati wa watu wakati wa kampeni za uchaguzi katika mji wa magharibi wa Japan wa Nara.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment