Israel itajibu baada ya Hamas kutoa mabaki ya miili ya mateka yasio sahihi – Netanyahu

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Hamas inadai inajitahidi kupata na kutambua mabaki yote, lakini inakosa vifaa vinavyohitajika kutokana na uharibifu mkubwa katika Gaza.

Netanyahu asema Israel itajibu baada ya Hamas kuwakabidhi miili ambayo sio ya mateka wao

h

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ametangaza kuwa Israel itachukua hatua baada ya Hamas kutoa mabaki ya binadamu ambayo hayakuwa ya yoyote ya wafungwa 13 wa Israeli waliopotea, akisema ni ukiukaji wa mpango wa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Mabaki hayo yalitambulika kuwa ni ya Ofir Tzarfati, ambaye tayari mwili wake ulikutwa mwanzoni mwa vita.

Hamas ilidai inatekeleza matakwa ya kusitisha mapigano na inajitahidi kupata na kutambua mabaki yote, lakini inakosa vifaa vinavyohitajika kutokana na uharibifu mkubwa katika Gaza.

Msemaji wa Hamas, Hazem Qassem, alisema kundi hilo litaendelea na juhudi zake zote kuhakikisha mabaki ya mateka yaliyobaki yote yanarudishwa.

Wakati huo huo, milipuko bado inaendelea kusikika Gaza huku majeshi ya Israeli yakikaribia kuharibu mahandaki ya Hamas, ambapo Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, alisema takriban 60% ya mahandaki bado ipo.

Serikali ya kijeshi ya Madagascar yateua Baraza la Mawaziri wengi wakiwa raia

G

Serikali ya Madagascar inayoongozwa na wanajeshi, ambayo ilipata madaraka mwanzoni mwa mwezi huu, imetangaza baraza la mawaziri siku ya Jumanne lililojumuisha mawaziri wengi raia, ikiwemo baadhi ya wapinzani wakuu wa rais aliyefukuzwa, Andry Rajoelina.

Uteuzi huu unaashiria hatua muhimu katika mzozo wa kisiasa wa Madagascar, huku wanajeshi wakiimarisha madaraka yake.

Kwa mujibu wa serikali ya mpito ya sasa imesema itashughulikia changamoto za kiuchumi na mgawanyiko wa kisiasa.

Wanajeshi walifanya mapinduzi mwanzoni mwa mwezi huu baada ya Rajoelina kukimbia kutoka kisiwa cha Bahari ya Hindi kufuatia wiki za maandamano yaliyoongozwa na vijana.

Kanali Michael Randrianirina alichukua wadhifa wa rais wa muda mfupi siku chache baadaye.

Hadi sasa, hakujakuwa na maandamano ya kupinga uteuzi wa baraza la mawaziri.

unaamini kuwa suala la Bahari ya Shamu ni la kisheria, kihistoria na kiuchumi – Abiy Ahmed

h

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amewaomba viongozi wakuu wa dunia ikijumuisha Marekani, China, Urusi, na Umoja wa Ulaya kusaidia juhudi za Uhabeshi za kupata upatikanaji wa Bahari Nyekundu, akieleza kuwa suala hilo ni la lazima na la kimsingi kwa taifa hilo.

Akizungumza na wabunge siku ya Jumanne, Bw. Abiy alisisitiza kuwa Uhabeshi inapendelea mazungumzo ya amani na tayari imeomba ushiriki wa kimataifa ili kusaidia kupata suluhisho la kidiplomasia.

Aidha, alihoji kisheria mchakato wa kihistoria uliosababisha Ethiopia kuwa bila bandari kufuatia uhuru wa Eritrea mwaka 1993.

Kabla ya hapo, Ethiopia ilikuwa na upatikanaji wa Bahari Nyekundu kupitia bandari kama Assab, ambayo baadaye ilijumuishwa Eritrea baada ya kujitenga.

Tangu wakati huo, Ethiopia imekuwa ikitegemea kwa kiasi kikubwa bandari za jirani yake mdogo Mashariki, Djibouti, kwa karibu zote za bidhaa zake zinazoingizwa na kusafirishwa nje ya taifa hilo.

Matamshi ya hivi karibuni ya Bw. Abiy yamezua mvutano na Eritrea, ambayo inaona mapendekezo yoyote ya kuangalia upya hali ya ardhi kama tishio.

Kama sehemu ya juhudi zake za kupata upatikanaji wa baharini, Uhabeshi ilisaini makubaliano ya awali na Somaliland mwanzoni mwa mwaka huu.

Mkataba huo, uliokusudiwa kuanzisha uwepo wa jeshi la majini na upatikanaji wa bandari, ulionekana na Somalia kama kitendo cha ukatili, kwani inachukulia Somaliland kama sehemu ya eneo lake la kiasili.

Makubaliano hayo yalisababisha mvutano wa kikanda na kuibua hofu ya kutokuwa na utulivu katika Pembe ya Afrika.

Ingawa makubaliano bado hayajafutwa rasmi, hatma yake bado haijulikani.

Mvutano unaoendelea kati ya Addis Ababa na Asmara umeibua hofu kuwa vita vipya vinaweza kuibuka kati ya nchi jirani hizi mbili.

Ni kipi kinachoendelea Sudan baada ya RSF kudhibiti el Fasher

Mamia kwa maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea
Maelezo ya picha,Mamia kwa maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea

Watafiti nchini Marekani wanasema wamepata ushahidi wa mauaji ya halaiki, baada ya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) kuudhibiti mji wa el-Fasher kutoka kwa jeshi la Sudan.

Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Yale inasema picha za satelaiti zinaonyesha makundi ya kile kinachoonekana kuwa miili ya binadamu karibu na magari ya RSF na ukuta unaozunguka jiji hilo.

Watafiti hao wanasema kuwa picha hizo pia zinathibitisha kuwa RSF imekamata nyadhifa zote za jeshi.

Pia wameona ushahidi wa shughuli za nyumba hadi nyumba na vizuizi vipya vya barabarani kote jijini.

Ripoti ya Yale inaonya kwamba mtindo wa ghasia unaonekana kulengwa kikabila sawa na ukatili mkubwa uliorekodiwa hapo awali katika maeneo mengine ya Darfur tangu mzozo huo uanze Aprili 2023.

Pia inasema maendeleo ya RSF, pamoja na upatikanaji wa kibinadamu wenye vikwazo, “huongeza hatari ya uhalifu dhidi ya ubinadamu au hata mauaji ya kimbari”.

Wakati huo huo, familia za waathiriwa wa Sudan zimezungumza na idhaa ya BBC.

“Tumeshuhudia jamaa zetu wengi wakiuawa,” mwanamume mmoja ambaye alipoteza mawasiliano na wanafamilia huko El-Fasher aliambia Idhaa ya BBC.

Anasema walikusanywa sehemu moja na kuuawa kufuatia kutekwa kwa jiji hilo.

Mawasiliano “yamekatika kabisa” katika Jimbo la Darfur Kaskazini, mkazi huyo anasema, kwa hivyo hajui nini kimetokea kwa wanafamilia ambao bado wako hai.

ChatGPT yatoa takwimu kuhusu watumiaji wanaoonyesha dalili za mawazo ya kujitoa uhai

gg

Kampuni ya OpenAI imechapisha takwimu mpya zinazokadiria idadi ya watumiaji wa ChatGPT wanaoonyesha dalili zinazoweza kuashiria dharura za kiafya ya akili, ikiwamo wazimu, kurukwa na akili na mawazo ya kujitoa uhai.

OpenAI imesema kuwa takriban asilimia 0.07 ya watumiaji wake hai katika kipindi cha wiki moja walionyesha dalili hizo, na kuongeza kuwa mfumo wake wa akili bandia (AI) umewekwa ili kutambua na kutoa majibu kwa mazungumzo nyeti yanayohusiana na hali hizi.

Ingawa kampuni inasisitiza kuwa matukio haya ni nadra sana, wakosoaji wameonyesha wasiwasi kuwa hata asilimia ndogo inaweza kumaanisha mamia ya maelfu ya watu kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa ChatGPT, ambao hivi karibuni walifikia milioni 800 wa watumiaji hai kwa wiki, kama alivyosema Mkurugenzi Mtendaji Sam Altman.

Ili kukabiliana na changamoto hii, OpenAI imeanzisha mtandao wa wataalamu wa afya ya akili na teknolojia kutoka duniani kote ili kutoa ushauri wa kitaalamu.

Katika tukio jingine lililotokea Agosti mwaka huu, mtu aliyeshutumiwa kwa mauaji na kujiua katika eneo la Greenwich, Connecticut, alitoa rekodi za masaa ya mazungumzo yake na ChatGPT, ambayo yanaonekana kuwa chanzo cha kuongezeka kwa mawazo potofu aliyokuwa nayo.

Profesa Robin Feldman, Mkurugenzi wa Taasisi ya Sheria na Ubunifu wa AI katika Chuo Kikuu cha California, anasema, “Watumiaji wengi wanakumbwa na kurukwa na akili inayohusiana na matumizi ya AI kutokana na chatbots kuunda udanganyifu thabiti wa uhalisia.”

Anasisitiza kuwa OpenAI inastahili sifa kwa uwazi wake na juhudi za kupambana na tatizo hili, lakini pia anabainisha kuwa “hata onyo la kina linaweza kutolewa, mtu aliye katika hatari ya kiafya ya akili huenda asiweze kulizingatia.”

Tanzania yaongoza uchumi wa kanda, Kenya na Rwanda zikibaki nyuma – ripoti ya AU

g

Uchumi wa Kenya umeendelea kusuasua ikilinganishwa na ule wa Tanzania katika eneo la Afrika Mashariki, hasa kutokana na utegemezi mkubwa wa mauzo ya bidhaa ghafi nje ya nchi jambo linalokwamisha ukuaji wa uchumi na kuongeza kiwango cha umaskini.

Hayo yamebainishwa katika Ripoti ya Ujumuishaji wa Bara la Afrika 2025 iliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU).

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla unafanya chini ya wastani wa bara katika juhudi za kuimarisha uchumi wake kupitia ubunifu, uongezaji thamani wa bidhaa na upanuzi wa sekta za uzalishaji.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kenya inajipata ikifanya vibaya zaidi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), huku uchumi wake ukiendelea kutegemea zaidi mauzo ya bidhaa ghafi badala ya bidhaa zilizoongezwa thamani.

Hali hiyo, ripoti inasema, imeathiri maendeleo ya viwanda na sekta ya uzalishaji nchini, jambo linalochangia upungufu wa ajira, kipengele muhimu katika kupunguza ukosefu wa ajira na umaskini.

Alama ya utofauti wa biashara katika EAC (0.3920) imebaki chini kidogo ya wastani wa bara la Afrika (0.4072).

Biashara nchini Kenya bado inatawaliwa na mauzo ya bidhaa ghafi (asilimia takribani 68 ya mauzo nje), huku mauzo ya bidhaa za viwandani (0.3420) yakiwa nyuma ya uagizaji wake (0.5986).

Kwa upande wa utofauti wa biashara, Tanzania inaongoza kwa alama 0.4457, ikifuatiwa na Burundi, kisha Kenya.

Nchi zinazofanya vibaya zaidi ni Uganda (0.2848), Rwanda (0.2241) na Sudan Kusini (0.2116), hali inayoonyesha pengo kubwa kati ya wingi wa biashara na kiwango cha ubunifu wa uchumi.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa biashara ya bidhaa za kati bado ni dhaifu, huku mitandao ya uzalishaji wa kikanda ikiwa haijakomaa ipasavyo.

Wataalamu wa Umoja wa Afrika wanapendekeza kuwa jumuiya ya Afrika mashariki EAC ichukue hatua mahsusi za kupunguza pengo la biashara kwa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara ndani ya eneo, kukuza uzalishaji wa viwandani, na kuhamasisha uongezaji thamani wa bidhaa.

“Kuimarisha minyororo ya thamani ya kikanda, hasa katika sekta za usindikaji wa mazao na viwanda vidogo, kunaweza kusaidia kupunguza pengo kati ya uagizaji na uuzaji nje. Uboreshaji wa njia kuu za usafirishaji kama vile Mombasa na Dar es Salaam ni muhimu kwa kuongeza ujumuishaji wa kiuchumi,” inasema ripoti hiyo.

Aidha, ripoti inabainisha kuwa nchi dhaifu kama Somalia na Sudan Kusini zinahitaji msaada maalumu unaojumuisha uwekezaji katika miundombinu na ushirikiano wa kiusalama, ili kuwezesha ushiriki wao kamili katika ujumuishaji wa kiuchumi wa bara.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment