Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Chalinee Thirasupa/Pool/AFP
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametoa mwito wa mazungumzo ya amani kufanyika mara moja ili kusitisha mapigano yanayoendelea Sudan.
Mwito wa Guterres unatolewa baada ya wanamgambo wa RSF kuuteka mji wa El Fasher jana Jumatatu. Katika taarifa, msemaji wa katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephan Dujarric, amesema Guterres analitaka jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF kuwasiliana na mjumbe wake wa Sudan Ramtane Lamamra,haraka kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka za kufikia makubaliano.
Wakati huo huo, Umoja wa Afrika umelaani visa vya ”Ukatili” na “uhalifu wa kivita” vinavyoripotiwa huko El Fasher.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya umoja huo, Mahmoud Ali Youssouf kupitia taarifa aliyoitoa kwenye mtandao wa kijamii wa X, amesema ana wasiwasi kuhusu machafuko na madai ya mauaji ya kikabila yanayoendelea huko El Fasher.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.