Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Mfalme wa Japan Naruhito mjini Tokyo: 27.10.2025Picha: Kazuhiro Nogi/Pool/AFP
Rais wa Marekani Donald Trump amewasili Japan siku ya Jumatatu katika siku ya pili ya ziara yake barani Asia.
Trump anatarajiwa siku ya Jumanne kukutana na Waziri Mkuu wa wa Japan Sanae Takaichi katika mkutano wenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Japan.
Ziara ya Trump barani Asia imekuwa pia fursa ya kusaini mikataba kadhaa ya kibiashara kabla ya kuhudhuria pia siku ya Jumatano mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya nchi za Asia-Pasifiki, APEC katika mji wa Gyeonju nchini Korea Kusini.
Trump atakamilisha ziara yake barani Asia kwa kufanya mkutano wa kilele na Rais wa China na Xi Jinping siku ya Alhamisi huko Korea Kusini ambapo viongozi hao wanalenga kutafuta suluhu ya miezi kadhaa ya vita vya kibiashara.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.