Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Mfalme Naruhito wa Japan mjini TokyoPicha: Kazuhiro Nogi – Pool/Getty Images
Rais wa Marekani Donald Trump amekutana Jumatatu mjini Tokyo na Mfalme Naruhito wa Japan.
Siku ya Jumanne Trump anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Sanae Takaichi katika mkutano wenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Japan.
Ziara ya Trump barani Asia imekuwa pia fursa ya kusaini mikataba kadhaa ya kibiashara, ambapo tayari Japan imetoa ahadi ya uwekezeji wa dola bilioni 550 chini ya makubaliano ya kupunguziwa ushuru wa bidhaa zake zinazoingia nchini Marekani.
Trump atahudhuria pia siku ya Jumatano mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya nchi za Asia-Pasifiki, APEC katika mji wa Gyeonju nchini Korea Kusini ambako pia anatarajiwa kukutana na Rais wa China na Xi Jinping siku ya Alhamisi. Trump na Xi wanalenga kutafuta suluhu ya miezi kadhaa ya vita vyao vya kibiashara.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.