Papa Leo kuzuru miji minane katika safari ya kwanza nje ya nchi kama papa

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Papa Leo XIV mwenye umri wa miaka 69 ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.
Maelezo ya picha,Papa Leo XIV mwenye umri wa miaka 69 ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.

Papa Leo atatembelea miji minane nchini Uturuki na Lebanon baadaye mwaka huu, Vatican ilisema Jumatatu ya tarehe 27 Mwezi Oktoba mwaka huu.

Itakuwa safari yake ya kwanza nje ya Italia kama papa, na anatarajiwa kutoa wito wa amani katika eneo lote.

Leo, papa wa kwanza wa Marekani, atazuru Uturuki kuanzia Novemba 27 hadi 30 na kisha atakuwa Lebanon kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 2.

Mtangulizi wa Leo Papa Francis alikuwa amepanga kuzuru nchi zote mbili lakini hakuweza kwenda kwa sababu ya afya yake kuwa mbaya.

Francis alifariki Aprili 21 na Leo alichaguliwa kuwa papa mpya Mei 8 na makadinali wa dunia.

Leo pia atakutana na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan katika mji mkuu Ankara, atatembelea Msikiti wa Blue huko Istanbul, na ataadhimisha Misa ya Kikatoliki katika uwanja wa Volkswagen Arena wa Istanbul.

Kusafiri ng’ambo kumekuwa sehemu kubwa ya upapa wa kisasa, huku mapapa wakitafuta kukutana na Wakatoliki wenyeji, kueneza imani, na kufanya diplomasia ya kimataifa.

Safari za kwanza za papa mpya kwa kawaida huonekana kama dalili ya masuala ambayo papa anataka kuangazia wakati wa utawala wake.

Uturuki na Lebanon ni nchi zenye Waislamu wengi, na Francis alitilia mkazo sana mazungumzo ya Waislamu na Wakatoliki wakati wa utawala wa miaka 12 uliojumuisha safari 47 nje ya nchi.

Kauli mbiu rasmi ya safari ya Leo Lebanon ni “Heri wapatanishi”.

Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon asema nyumba yake inashambuliwa

,

Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon Issa Tchiroma Bakary anasema watu wawili wameuawa na wavamizi mbele ya nyumba yake huko Garoua, huku mvutano ukizidi baada ya uchaguzi.

Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii, alisema raia waliopiga kambi nje ya nyumba yake walikuwa wakipigwa risasi “karibu.” “Heri mniue lakini nitaikomboa nchi hii kwa njia yoyote ile,” Tchiroma Bakary alitangaza, akielezea vitendo hivyo kama “udubutu uliyopitiliza wa uvunjaji wa sheria”

Aliweka mtandaoni picha na video ya watu wenye silaha wakiwa juu waliokuwa juu ya nyumba wakifyatua risasi mara kadhaa.

BBC haijathibitisha uhalisia wa video na picha hizo, au majeruhi waliotajwa.

Matukio haya yanajiri baada ya Rais aliye madarakani Paul Biya akitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa takribani asilimia 54 ya kura

Upinzani ulitangazwa kuwa wa pili, kwa asilimia 35.

Maandamano yameripotiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa huku baadhi ya raia wakihofia kuwa taifa hilo la Afrika ya Kati lhuenda likatumbukia katika mgogoro wa baada ya uchaguzi.

.

Uchaguzi Cameroon: Maandamano ya vurugu yazidi huko Douala – ripoti

Maandamano yamezuka huko Douala, mji mkuu wa kiuchumi wa Cameroon, kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.

Picha zilizochapishwa na kituo cha habari cha Mimi Mefo Infos, zinaonyesha watu kadhaa wakikimbia barabarani, wakiimba jina la Issa Tchiroma Bakary kwa pamoja.

Shirika la Habari la Cameroon lilichapisha video, nje inayoonyesha jengo la baraza lililoharibiwa, linalodaiwa kushambuliwa na waandamanaji.

Rais mteule Paul Biya bado hajawahutubia wananchi wa Cameroon baada ya kuchaguliwa tena Jumatatu, lakini chama tawala kimepongeza ushindi wake “chini ya ishara ya ukuu na matumaini” katika machapisho ya mtandaoni.

Hakujawa na maoni yoyote kutoka kwa serikali kuhusu ripoti kwamba watu wenye silaha wamefyatua risasi na kuua watu wawili karibu na nyumba ya mshindi wa pili Issa Tchiroma Bakary.

Akizungumza katika kumuunga mkono rais siku ya Jumatatu, mpiga kura kwa jina Serge Pascal Eyango aliambia shirika la habari la Reuters:

“Kati ya mikoa 10 ya Cameroon, Rais wa Jamhuri alishinda saba. Na mgombea ambaye alijaribu kufanya jambo muhimu katika mikoa mitatu, Issa Tchiroma [Bakary], pongezi kwake. “Lakini… inathibitisha ni kwa kiasi gani watu wa Cameroon bado wanamuunga mkono mkuu wao wa nchi. Hilo ndilo jambo muhimu. Yeye ni mtu wa amani, sura inayounganisha, baba kwa watoto, na bado tuna matumaini makubwa kwake. Hilo ndilo tu tulilotarajia.”

Kenya, Tanzania kukabiliwa na dhoruba ya tropiki inayojulikana kama ‘Chege’ – KMD

Idara ya hali ya hewa nchini Kenya yatoa onyo ya mvua kubwa inayoambatana na upepo mkali pwani ya Afrika Mashariki
Maelezo ya picha,Idara ya hali ya hewa nchini Kenya yatoa onyo ya mvua kubwa inayoambatana na upepo mkali pwani ya Afrika Mashariki

Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya (KMD) imetahadharisha kwamba mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika pwani ya kusini kutokana na dhoruba ya kitropiki inayoitwa “Chenge”.

Dhoruba hii, inayojulikana kama Chenge residual depression, ni eneo la shinikizo la chini katika Bahari ya Hindi, likisogea magharibi kwa kasi ya 11 km/h, takriban kilomita 500 kaskazini mwa Madagascar, likiwa na upepo wa 55 km/h, milipuko hadi 75 km/h, na shinikizo karibu na 1000 hPa.

KMD imesema katika taarifa Jumapili kuwa dhoruba inaendelea kudhoofika wakati ikisogea magharibi kupitia Kituo cha Kaskazini cha Mozambique, lakini ukaribu wake na pwani unaweza kuathiri hali ya hewa nchini Kenya na baadhi ya maeneo ya Tanzania.

“Mvua kubwa inatarajiwa kunyesha sehemu mbalimbali za nchi, huku upepo mkali wa zaidi ya 25 knots uwezekano kufika pwani ya kusini Jumatatu na Jumanne,” taarifa hiyo ilisema.

Wakazi wa maeneo haya, hasa wanaojihusisha na shughuli za baharini, wametakiwa kuwa makini, kuwa macho, na kuchukua tahadhari zote zinazohitajika.

Mali yafunga shule na vyuo vikuu nchini kote kufuatia uhaba mkubwa wa mafuta

Milolongo mirefu ya magari na watu imeshuhudiwa katika vituo vya mafuta vya Bamako katika wiki za hivi karibuni
Maelezo ya picha,Milolongo mirefu ya magari na watu imeshuhudiwa katika vituo vya mafuta vya Bamako katika wiki za hivi karibuni

Serikali ya Mali imesimamisha masomo katika shule na vyuo vikuu vyote nchini humo kufuatia uhaba mkubwa wa mafuta uliosababishwa na wanamgambo kuzuia uingizaji wa bidhaa za mafuta nchini.

Waziri wa Elimu, Amadou Sy Savane, ametangaza kuwa taasisi zote za elimu zitasalia kufungwa hadi tarehe 9 Novemba, akieleza kuwa walimu, wahudumu na wanafunzi wamekosa usafiri kutokana na hujuma zinazofanywa na wanamgambo hao.

Waziri Savane aliongeza kuwa serikali inafanya kila juhudi kumaliza mzozo huo ili masomo yaanze tena kuanzia tarehe 10 mwezi Novemba.

Kwa wiki kadhaa sasa, Mali imekumbwa na uhaba wa mafuta, hasa katika mji mkuu Bamako, baada ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu wanaohusishwa na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda kuanza kushambulia malori ya mafuta katika barabara kuu za nchi hiyo.

Kwa kuwa Mali haina bandari, bidhaa zote za mafuta husafirishwa kwa malori kutoka nchi jirani kama Senegal na Ivory Coast.

Hali hiyo imesababisha foleni ndefu katika vituo vya mafuta jijini Bamako, huku barabara ambazo kwa kawaida huwa na shughuli nyingi sasa zikiwa kimya na tupu.

Serikali ya kijeshi inayoongozwa na Jenerali Assimi Goïta, ambaye alitwaa madaraka kupitia mapinduzi ya mwaka 2021, iliwahakikishia raia hivi karibuni kwamba uhaba huo wa mafuta ni wa muda mfupi.

Hata hivyo, hali imeendelea kuzorota zaidi ya ilivyotarajiwa. Wiki iliyopita, ubalozi wa Marekani mjini Bamako ulitangaza kuwa utaondoa wafanyakazi wake wasio wa lazima pamoja na familia zao kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi wa kiusalama na athari za uhaba huo wa mafuta, ambao umelemaza usafiri na huduma za umeme nchini.

Licha ya jeshi kushika hatamu za uongozi, wanamgambo wenye misimamo mikali wameendelea kudhibiti maeneo mengi ya kaskazini na mashariki mwa Mali.

Baada ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani (MINUSMA) na vikosi vya Ufaransa kuondoka nchini humo, serikali ya Jenerali Goïta sasa inategemea mamluki wa Urusi kushughulikia masuala ya usalama nchini humo.

Vikosi vya kimataifa havitakubali kulazimisha amani Gaza – Mfalme wa Jordan

Mfalme wa Jordan
Maelezo ya picha,Mfalme wa Jordan

Nchi nyingi hazitakubali jukumu la “kulazimisha” amani Gaza endapo zitatumwa chini ya mpango wa kusitisha mapigano wa rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Mfalme Abdullah wa Jordan katika mahojiano maalum na BBC.

Kupitia mpango huo wa amani wa vipengele 20, Marekani ilipendekeza kwamba mataifa ya Kiarabu na washirika wa kimataifa yatoe vikosi maalum vya uthabiti ambavyo “vitatoa mafunzo na msaada kwa vikosi vya polisi vya Wapalestina vilivyothibitishwa Gaza, na vitashauriana na Jordan na Misri, ambazo zina uzoefu mkubwa katika masuala ya usalama wa kikanda.”

Mpango huo pia unaitaka Hamas kuvunja silaha na kuachia madaraka ya kisiasa katika eneo hilo.

“Ni mamlaka gani yatakayotolewa kwa vikosi vya usalama ndani ya Gaza? Tunatumaini kwamba itakuwa operesheni ya kulinda amani, kwa sababu kama itakuwa ya kulazimisha amani, hakuna nchi itakayopenda kujihusisha nayo,” alisema Mfalme Abdullah.

Katika mahojiano hayo maalum kwa kipindi cha BBC Panorama, Mfalme huyo alisema Jordan na Misri ziko tayari kusaidia katika kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Wapalestina.

“Kulinda amani ni kuwasaidia polisi wa wenyeji yaani Wapalestina jambo ambalo Jordan na Misri ziko tayari kulifanya kwa wingi, ingawa linahitaji muda. Lakini ikiwa tutakuwa tunazunguka Gaza kwenye doria tukiwa na silaha, hiyo si hali ambayo taifa lolote lingependa kujihusisha nayo,” aliongeza.

Kauli za Mfalme Abdullah zinaakisi wasiwasi wa Marekani na mataifa mengine kuhusu hatari ya kuvutwa katika mzozo unaoendelea kati ya Hamas na Israel, au kati ya Hamas na makundi mengine ya Kipalestina.

Mfalme huyo pia alisisitiza kwamba Jordan haitatuma wanajeshi wake Gaza, akieleza kuwa nchi yake “iko karibu sana kisiasa” na mzozo huo.

Zaidi ya nusu ya wananchi wa Jordan ni wenye asili ya Kipalestina, na kwa miongo kadhaa taifa hilo limewapokea wakimbizi wa Kipalestina wapatao milioni 2.3 waliokimbia vita vya awali na Israel idadi kubwa zaidi katika eneo hilo.

Alipoulizwa kama ana imani kwamba Hamas itatekeleza ahadi yake ya kuachana na siasa katika ukanda wa Gaza, alijibu: “Siwajui moja kwa moja, lakini wale wanaofanya kazi kwa karibu nao – Qatar na Misri – wana matumaini makubwa kwamba watatii makubaliano hayo.”

Mfalme Abdullah alionya kuwa mustakabali wa amani Mashariki ya Kati unategemea kutatuliwa kwa mzozo wa muda mrefu kati ya Israel na Wapalestina.

“Iwapo hatutatua tatizo hili, iwapo hatutapata mustakabali wa pamoja kwa Waisraeli na Wapalestina na kuimarisha uhusiano kati ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu na Israel, basi tutaangamia,” alisema.

Kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ya Trump kulifuatwa na kuachiliwa kwa mateka 20 wa Kiyahudi waliokuwa hai kutoka Gaza, huku juhudi zikiendelea kurejesha miili ya waliouawa.

Israel nayo iliwaachilia wafungwa 250 wa Kipalestina waliokuwa wamehukumiwa kwa makosa mbalimbali, yakiwemo mauaji na mashambulizi dhidi ya raia wa Israel, pamoja na takribani wafungwa 1,700 kutoka Gaza waliokuwa wakizuiliwa bila mashitaka.

UN yaomba njia salama kwa raia waliokwama katika mji wa el-Fasher, Sudan

Mamia kwa maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao kwa sababu ya mzozo nchini Sudan
Maelezo ya picha,Mamia kwa maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao kwa sababu ya mzozo nchini Sudan

Umoja wa Mataifa umezitaka pande zinazopigana nchini Sudan kuhakikisha raia waliokwama mjini el-Fasher wanapatiwa njia salama ya kuondoka, baada ya wapiganaji wa kundi la Rapid Support Forces (RSF) kutangaza kuwa wametwaa udhibiti wa kambi kuu ya jeshi katika mji huo.

Jeshi la Sudan halijathibitisha kupoteza kambi hiyo, jambo ambalo, likithibitishwa, litakuwa ushindi mkubwa kwa RSF katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alisema mapigano hayo mapya ni “ongezeko baya mno la machafuko,” na kuongeza kuwa mateso wanayopitia raia ni “yasiyovumilika,” kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

El-Fasher, ambayo ni ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan katika eneo pana la magharibi mwa Darfur, imekuwa chini ya mzingiro wa RSF na washirika wake kwa zaidi ya miezi 18.

Mapigano makali yamezuka tangu Jumamosi, baada ya wapiganaji wa RSF kuteka makazi ya gavana wa jimbo la Kaskazini mwa Darfur.

Video zilizothibitishwa na BBC kutoka mitandao ya kijamii zinaonyesha wapiganaji wa RSF wakisherehekea baada ya kuteka makao makuu ya jeshi mjini el-Fasher.

RSF inadai kudhibiti mji mzima, lakini washirika wa kijeshi wa serikali katika eneo hilo wanasema mapigano bado yanaendelea katika baadhi ya mitaa.

Kundi hilo limekosolewa kwa kushambulia raia kwa mabomu ya angani na kuwazuilia takribani watu 250,000, baada ya kuuzungushia mji huo ukuta wa udongo, hali iliyowaacha wengi katika njaa kali na kukosa msaada wa kibinadamu.

Mji wa el-Fasher sasa unatajwa kuwa moja ya maeneo yenye mapigano makubwa zaidi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan, ambapo Umoja wa Mataifa umeueleza kama “kitovu cha mateso.”

Afisa Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, alisema ameshtushwa sana na taarifa za vifo na mateso ya raia.

“Wapiganaji wanapozidi kusonga kuelekea katikati mwa mji na njia za kutoroka zikifungwa, mamia ya maelfu ya raia wamekwama wakiwa na hofu ya kushambuliwa, wakikabiliwa na njaa, bila chakula, huduma za afya, wala usalama,” alisema Fletcher kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.

Tangu machafuko kuanza, zaidi ya watu 150,000 wameuawa kote nchini, huku takribani watu milioni 12 wakiyakimbia makazi yao, hali ambayo Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni moja ya migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani.

Kwa sasa, jeshi la Sudan linadhibiti maeneo mengi ya kaskazini na mashariki mwa nchi, huku el-Fasher ikiwa mji wa mwisho mkubwa katika Darfur uliokuwa bado chini ya udhibiti wa serikali na washirika wake.

RSF, kwa upande wake, inadhibiti karibu eneo lote la Darfur na sehemu kubwa ya mkoa wa Kordofan, na imewahi kutangaza azma ya kuunda serikali pinzani mjini el-Fasher pindi itakapodhibiti eneo hilo kikamilifu.

Ufikiaji wa mtandao umetatizwa nchini Cameroon

Hali ilivyo nchini Cameroon
Maelezo ya picha,Hali ilivyo nchini Cameroon

Muunganisho wa intaneti umekuwa si dhabiti katika siku za hivi majuzi nchini Cameroon.

Siku ya Alhamisi, mfuatiliaji wa mtandao wa NetBlocks aliripoti “kuvurugika kwa muunganisho wa intaneti” ambao unaweza “kuzuia utangazaji wa matukio mashinani huku kukiwa na wito wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais huku Rais Biya akitafuta kuongeza miaka 43 madarakani”.

Siku hiyo hiyo, kampuni ya kitaifa ya mawasiliano ya Camtel ilisema kumekuwa na “tukio la kiufundi”.

Wakati huo huo, barabara za jiji la Bamenda, magharibi mwa nchi inayozungumza Kiingereza, hazina watu na raia wako ndani ya nyumba.

Mapema sana asubuhi ya leo, mashabiki wa michezo walikuwa mitaani; wengine wakitembea kwa kasi huku wengine wakikimbia.

Hata hivyo, kufikia saa 10:00 (09:00 GMT) mitaa ilikuwa haina watu.

Wanajeshi wapo kwenye makutano yote makubwa.

Uwepo wao unaonekana unanuiwa kuzuia maandamano yoyote yanayohusiana na uchaguzi.

Kwa sasa, mawingu meusi yanaonekana yakikusanyika, kuashiria mvua mchana.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment