Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Kilmar Abrego Garcia anayetarajiwa kuhamishwa na Marekani hadi LiberiaPicha: Seth Herald/REUTERS
Serikali ya Marekani imesema inataka kumhamishia nchini Liberia raia wa Salvador Kilmar Abrego Garcia kufikia mwishoni mwa mwezi huu. Hatua hizo imekuja katikati mwa mzozo kuhusu mpango wa uhamiaji wa Rais Donald Trump .
Katika ombi lililowasilishwa katika mahakama ya Maryland jana Ijumaa, mawakili wa serikali walisema wameichagua Liberia kama eneo la kumhamishia mhamiaji huyo kwa sababu haikuwa katika orodha ya nchi ambazo mawakili wa Abrego Garcia walikuwa wameikataa.
Mawakili hao wamesema Liberia ni taifa lenye demokrasia iliyostawi na mojawapo ya washirika wa karibu wa Marekani katika bara la Afrika.
Serikali pia imebainisha kuwa Liberia ni nchi inayozungumza Kiingereza na imejitolea kuwachukulia wakimbizi kibinadamu.
Mawakili wa Abrego Garcia hawakujibu mara moja ombi la tamko kuhusu hali hiyo.
Kesi ya Abrego Garcia, ambaye mwezi Machi alihamishiwa kimakosa hadi El Salvador na kisha kurejeshwa Marekani mwezi Juni, imewavutia wengi wanaopinga juhudi za Trump za kuwahamisha wahamiaji wengi kutoka Marekani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.