Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip ErdoganPicha: DHA
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema Marekani na mataifa mengine yanapaswa kuchukua hatua zaidi kuishinikiza Israel kusitisha ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza.
Akiwa njiani kurejea kutoka Oman, Erdogan alisema kundi la Hamas linaheshimu makubaliano hayo, na kwamba Uturuki iko tayari kuunga mkono kikosi kazi kinachopangwa kwa ajili ya Gaza.
Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alisema hatua nzuri zimepigwa katika utekelezaji wa mpango wa amani wa Marekani kwa Gaza, na kueleza matumaini kwamba mazungumzo hayo yataendelea kuleta matokeo chanya.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.