Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamepelekwa rasmi nchini Tanzania kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.
Hatua hiyo inafuatia mwaliko wa Serikali ya Tanzania ambao ni sambamba na maagizo ya Baraza la EAC linalohitaji Jumuiya hiyo kufuatilia uchaguzi wa nchi zote wanachama.
Kiongozi wa ujumbe huo ambaye pia ni makamu wa rais wa zamani wa Uganda Dkt Speciosa Wandira Kazibwe alizungumza wakati wa uzinduzi wa wa misheni hiyo.
“Kama jumuiya iliyoanzishwa juu ya kanuni za utawala bora, sheria, na heshima kwa haki za binadamu, EAC inazingatia uchaguzi wa kuaminika kama msingi wa demokrasia na ujumuishaji wa kikanda,” alisema Dkt Speciosa Wandira Kazibwe.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa EAC, Mhe. Veronica Nduva, alisema kuwa misheni hiyo itatoa taarifa ya awali muda mfupi baada ya uchaguzi, ikifuatiwa na ripoti kamili ya mwisho. “Ripoti hizi zitawasilisha tuliyobaini na kutoa mapendekezo yenye lengo la kuimarisha michakato ya uchaguzi ya baadaye katika eneo hilo.”
Waangalizi pia watakuwa na fursa ya kutangamana na washikawadau wa uchaguzi, kufuatilia shughuli za kampeni za mwisho, na kufuatilia shughuli hiyo inavyoendelea katika vituo vya kupigia kura, upigaji kura, uhesabu wa kura, na shughuli ya utangazaji matokeo ya uchaguzi.
Uchaguzi mkuu wa Tanzania utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025, ambapo raia watakuwa na fursa ya kumchagua Rais, wabunge na madiwani.
Kikosi cha usalama cha Gaza kujumuisha nchi ambazo Israeli ‘inaziridhia,’ Rubio anasema

Kikosi cha usalama cha kimataifa kitakachowekwa Gaza chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano kitalazimika kuundwa na nchi ambazo Israel “inaziridhia”, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema Ijumaa wakati wa ziara yake nchini Israel.
Rubio aliongeza kuwa mustakabali wa utawala wa Gaza bado unahitaji kufanyiwa kazi kati ya Israel na mataifa washirika lakini hauwezi kujumuisha Hamas, akiongeza kuwa jukumu lolote linaloweza kutekelezwa na Mamlaka ya Palestina bado halijaamuliwa.
Takriban watu 4,400 walidhulumiwa na makasisi nchini Italia, kundi la waathiriwa linadai

Takriban watu 4,400 wamedhulumiwa na makasisi wa Kikatoliki nchini Italia katika kesi zilizoripotiwa tangu 2020, kikundi cha waathiriwa kilidaiwa siku ya Ijumaa, na kuongeza shinikizo kwa maaskofu kukabiliana na shida ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikikumba imani kubwa zaidi ya Kikristo ulimwenguni.
Idadi hiyo isiyo rasmi ya Rete l’Abuso, kundi kubwa zaidi la waathiriwa wa unyanyasaji wa kanisa nchini Italia, inatokana na walioyapitia waathiriwa, vyanzo vya mahakama na kesi zilizoripotiwa na vyombo vya habari, mwanzilishi wa kundi hilo Francesco Zanardi alisema.
Rete l’Abuso haikusema kesi zinazodaiwa kuwa unyanyasaji zilitokea kwa kiasi gani.
Mkutano wa Maaskofu wa Italia (CEI), ambao ulikosolewa na tume ya kuwalinda watoto ya Vatican wiki iliyopita, haukutoa maoni yoyote juu ya matokeo hayo, msemaji alisema.
Papa Leo, ambaye alikutana na manusura wa unyanyasaji wa kingono na makasisi kwa mara ya kwanza wiki hii, amewaambia maaskofu wapya zaidi wa Kanisa kutoficha madai ya utovu wa nidhamu. Mtangulizi wake, hayati Papa Francis, alilipa suala hilo kipaumbele katika utawala wake wa upapa wa miaka 12, na matokeo yakawa mchanganyiko.
Trump aonya Israeli haitaungwa mkono na Marekani ikiwa itanyakua Ukingo wa Magharibi

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali zaidi kwa Israel kuhusu mipango yake ya kunyakua Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, akisema kwamba hatua hiyo “itasababisha kutoungwa mkono na Marekani”, hata kama utawala wake ulijaribu kusitishaji vita vyake huko Gaza.
Matamshi hayo, yaliyochapishwa Alhamisi na jarida la Time, yalitokana na mahojiano ya Oktoba 15 yaliyofanyika siku chache baada ya mapatano ya Gaza yaliyosimamiwa na Marekani kuanza kutekelezwa.
Trump, ambaye suala la utulivu Mashariki ya Kati limekuwa sehemu kuu ya sera yake ya kigeni, hakuwa na shaka.
“Haitatokea,” alisema alipoulizwa kuhusu wito wa Israel kunyakua Ukingo wa Magharibi wa Palestina, unaokaliwa kwa mabavu tangu 1967.
“Haitatokea kwa sababu nilishazungumzia hilo kwa nchi za Kiarabu. Israel itapoteza uungwaji mkono wake kutoka kwa Marekani ikiwa hilo litatokea.”
Onyo lake linajitokeza wakati Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio na Makamu wa Rais JD Vance wote walipotembelea Israel wiki hii huku kukiwa na msukosuko wa kisiasa mjini Jerusalem na kuzuka kwa ghasia katika Ukingo wa Magharibi.
Rais wa Ecuador asema kuna mtu aliyejaribu kumtilia sumu

Rais wa Ecuador amesema mtu alijaribu kumtilia sumu kwa kuweka kemikali tatu za kiwango cha juu kwenye chokoleti na jamu.
Daniel Noboa alisema timu yake ina ushahidi wa kuthibitisha madai hayo, ingawa bado hajatoa ushahidi wowote hadharani.
Kiongozi huyo wa Amerika Kusini aliiambia CNN Alhamisi kwamba anaamini kuwa “haiwezekani” kwamba kemikali hizo tatu zingepatikana zikiwa kwa viwango vya juu katika vitu vyote kwa bahati mbaya.
Maoni yake yanawadia kufuatia mapigano makali nchini Ecuador kuhusu kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta chini ya urais wake. Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kati ametoa amri ya msako wa kijeshi dhidi ya magenge ya dawa za kulevya, lakini pia amekabiliwa na shutuma za kuwalenga waandamanaji.
Uingereza kushinikiza washirika kutoa silaha za masafa marefu kwa Ukraine

Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer atawasihi washirika wa Ukraine kuipatia nchi hiyo silaha za masafa marefu zaidi kushambulia Urusi. Rais Zelensky anatembelea Uingereza leo.
Starmer atakuwa mwenyeji wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pamoja na kile kinachoitwa “muungano wa walio tayari”, unaojumuisha zaidi ya washirika 20 wa Ukraine ambao wameahidi kutoa ulinzi wa kiusalama kwa Kyiv mara tu usitishaji vita utakapokamilika.
Zelensky amekuwa akiomba kwa wiki kadhaa apewe silaha zaidi za masafa marefu kutoka Magharibi, hatua ambayo Urusi imeonya kuwa itaongeza mzozo huo.
Kiongozi wa Ukraine anasafiri kutoka Brussels, ambako alikutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi kutafuta msaada wa kifedha.
EU yaapa kuendelea kuiunga mkono Ukraine

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakubaliana kuisaidia Ukraine kifedha katika kipindi kingine cha miaka miwili.
Lakini hata hivyo wameshindwa kutoa mamilioni ya fedha za Urusi zilizozuiwa ili kutoa ufadhili wa ulinzi wa nchi hiyo
Katika mkutano wao wa jana viongozi hao waliahirisha uamuzi wao wa kutumia kiasi ya Euro bilioni 140 za mali ya Urusi zinazoshikiliwa nchini Ubelgiji hadi hapo Desemba.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameeleza mkutano huo wa Ubelgiji kwamba hatua hiyo italeta matokeo chanya.
”Ningependa kuwashukuru viongozi wote wa Ulaya kwa misimamo yao thabiti kupitia vikwazo waliyoweka,” alisema.
Mkutano huo wa Brussels ulifanyika jana wakati kukitarajiwa kufanyika mkutano mwingine huko London ambako Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kuwahimiza viongozi wa Ulaya kuongeza kupeleka vifaa vya kijeshi nchini Ukraine.
Polisi wakabiliana na aafuasi wa upinzani Cameroon
Maafisa wa usalama kaskazini mwa Cameroon wamekabiliana na wafuasi wa chama cha upinzani waliokuwa wakiandamana kumuunga mkono mgombea urais Tchiroma Bakary aliyejitangaza mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 12 mwezi huu wa Oktoba.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamefunga barabara kwa mawe na kuwasha moto.
Bwana Bakary amewataka wafuasi wake kuandamana iwapo Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo yaliyochakachuliwa.
Matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais yanatarajiwa kutangazwa na na Tume ya Uchaguzi Jumatatu ijayo.
Matokeo ya awali yanaashiria huenda Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 92 akaendelea kuliongoza taifa hilo ambapo amekuwa madarakani kwa miaka 43 tayari.
Serikali imetoa wito wa kuwepo utulivu kuelekea Jumatatu.
Chama cha Kikomunisti cha China chawatimua majenerali wakuu kazini

Chama cha Kikomunisti cha China kimewafukuza majenerali tisa wakuu katika mojawapo ya misako yake maiubwa ya umma dhidi ya jeshi katika miongo kadhaa.
Maafisa wakuu tisa walishukiwa kufanya uhalifu mkubwa wa kifedha, taarifa iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya China ilisema.
Wengi wao walikuwa majenerali wa nyota tatu na sehemu ya Kamati Kuu ya maamuzi ya chama.
Pia wamefukuzwa kutoka kwa jeshi. Ingawa taarifa hiyo ilionyesha hatua hiyo kama sehemu ya harakati ya kupambana na ufisadi, wachambuzi wanasema inaweza pia kuonekana kama uamuzi wa kisiasa.
Hatua hiyo inajiri mkesha wa kikao cha wajumbe wa chama hicho ambapo Kamati Kuu itajadili mpango wa maendeleo ya uchumi wa nchi na kuwapigia kura wanachama wapya.
Kati ya hao tisa, He Weidong alichukuliwa kuwa afisa wa pili wa cheo cha juu katika jeshi la China, baada ya Rais Xi Jinping ambaye ni mwenyekiti wa CMC.
He Weidong alionekana mara ya mwisho mwezi Machi, na kutoweka kwake machoni mwa watu kulichochea uvumi kwamba alikuwa akichunguzwa kama sehemu ya mchakato wa kuwaondoa maafisa kijeshi wa ngazi ya juu serikalini.
Rais wa Ivory Coast, Ouattara 83, anawania muhula wa nne kiti cha urais

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anawania muhula wa nne katika uchaguzi wa siku ya Jumamosi, akiahidi kuendeleza ukuaji thabiti huku wakosoaji wakilaani kile wanachoeleza kama jitihada za serikali yake za kukandamiza upinzani.
Uchaguzi katika nchi hiyo mzalishaji mkubwa wa kakao duniani unawakutanisha Ouattara, 83, dhidi ya mawaziri wawili wa zamani wa serikali pamoja na mke wa zamani na msemaji wa zamani wa mtangulizi wake, Laurent Gbagbo.
Ouattara ndiye mgombea pekee anayeungwa mkono na chama chenye nguvu cha kisiasa, na hivyo kumfanya kuwa kipenzi wengi.
Wapinzani wengine wawili mashuhuri, Gbagbo na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Credit Suisse Tidjane Thiam, walizuiwa kushiriki.
Ouattara, ambaye amepuuzilia mbali wasiwasi kuhusu umri na afya yake, aliingia madarakani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi minne baada ya Gbagbo kukataa kushindwa katika uchaguzi wa 2010.
Mwanabenki wa zamani wa kimataifa na naibu mkurugenzi mkuu wa IMF, Ouattara amesaidia kuiweka Ivory Coast miongoni mwa nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi katika kanda hiyo.
Amesimamia mageuzi ya kikatiba yaliyomruhusu kukwepa ukomo wa mihula miwili, na kuibua hasira ya wapinzani wake.
Madaktari wa Gaza wakabiliana na changamoto za kuchunguza miili iliyorejeshwa na Israel

Kwenye chumba kimoja tu, bila vifaa vya uchunguzi wa DNA au mashine za kuhifadhi baridi, kikosi cha uchunguzi wa maiti katika hospitali ya Nasser mjini Gaza kinakabiliana na changamoto zinazotokana na amani.
Katika muda wa siku kumi na moja zilizopita, miili 195 imerejeshwa Gaza na mamlaka ya Israel, badala ya miili 13 ya mateka wa Israel, chini ya masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya Donald Trump.
Picha zilizotolewa na mamlaka za afya za Gaza zinaonyesha baadhi ya miili imeharibika vibaya, wakiwa wamevaa nguo za kiraia au wakiwa nusu uchi isipokuwa chupi, wengine wakiwa na dalili nyingi za majeraha.
Wengi wana mikono iliyofungwa nyuma ya mgongo, na madaktari wanasema baadhi ya miili ilifika ikiwa imefunikwa macho au kamba imefungwa kwa shingo zao.
Kikosi cha uchunguzi wa maiti katika hospitali ya Nasser kinajitahidi, bila rasilimali nyingi, kujibu maswali makubwa kuhusu ukandamizaji, dhuluma na utambulisho wa maiti.
Kiongozi wa kitengo hicho, Dkt. Ahmed Dheir, alisema mojawapo ya changamoto zao kubwa ni ukosefu wa nafasi ya kuhifadhi maiti kwa chumba kinachohitaji jokofu kuzuia miili kuoza.
Miili inafika Gaza ikiwa imeganda kabisa na inaweza kuchukua siku kadhaa kuyeyuka, jambo linalotoa changamoto hata kwa mbinu za msingi za utambulisho kama historia ya meno, uchunguzi wa kina au upasuaji wa maiti (autopsy).
“Hali ni ngumu sana,” alisema. “Kama tutangojea miili iyayuke baridi, mchakato wa kuoza huanza mara moja, kutuweka katika nafasi isiyowezekana [kwa sababu] tunapoteza uwezo wa kuchunguza mabaki hayo ipasavyo. Hivyo, njia yenye ufanisi zaidi ni kuchukua sampuli na kuripoti hali ya miili kama ilivyo.”
BBC imezungumza na wataalamu watatu wa uchunguzi wa maiti nje ya eneo hilo, ikiwemo mtaalamu mmoja wa ukandamizaji, kujifunza kuhusu michakato ya matibabu inayohusika katika uchunguzi wa aina hii wote walikubaliana kuwa kuna maswali magumu kujibiwa bila kufanya upasuaji wa maiti.
Dkt. Alaa al-Astal, mmoja wa kikosi cha uchunguzi wa maiti katika hospitali ya Nasser, alisema baadhi ya miili iliyo wasili ilionyesha “dalili za ukandamizaji”, kama vile alama za mabaka na mashimo kutokana na kufungwa kwa mikono na vidole vya miguu.
“Kulikuwa na visa vya kutisha sana, ambapo kufungwa kulikuwa kwa nguvu kiasi kwamba damu haifikii mikono, ikisababisha uharibifu wa tishu na dalili wazi za shinikizo kuzunguka mikono na vidole vya miguu,” alisema.
Dkt. Astal pia alitaja vitambaa vilivyo fungwa kwa shingo za baadhi ya miili kuwa vinahitaji uchunguzi zaidi.
“Ili kubaini kama kifo kilitokana na kupigwa kifungo au kuteswa, ingehitajika kufanya upasuaji wa maiti, lakini kwa kuwa mwili ulikuwa umegandishwa, haukufanyiwa uchunguzi wa ndani.”
Marekani yazindua mpango wa msamaha kwa wapiganaji wa Gaza watakaoweka silaha chini

Serikali ya Marekani imezindua mpango mpya wa kuanzisha vituo vya ‘mapatano ya hiari’ katika Ukanda wa Gaza, utakaowapa wapiganaji wanaokubali kusalimisha silaha zao fursa ya msamaha na urejeo salama katika maisha ya kiraia.
Ili kufanikisha hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amewasili nchini Israeli siku ya Alhamisi kwa ajili ya kutekeleza mpango wa amani wa vipengele 20 wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Kuwasili kwa Rubio kunafuatia kuondoka kwa Makamu wa Rais J.D. Vance, huku maafisa waandamizi wa Ikulu ya White House pamoja na mkwe wa Rais Trump, Jared Kushner, wakihitimisha ziara zao nchini humo.
Wote wanashiriki katika jitihada za kudumisha usitishaji vita wa siku 13 kati ya Israeli na harakati ya Kipalestina ya Hamas, miaka miwili baada ya vita vilivyoitikisa Mashariki ya Kati.
Katika hatua nyingine, serikali ya Israeli imepitisha kwa kura ya awali mswada wa kutekeleza sheria za Israeli katika Ukingo wa Magharibi hatua ambayo wachambuzi wanaiona kama jaribio la kuinyakua ardhi inayotazamwa na Wapalestina kuwa sehemu ya taifa lao huru la baadaye.
Kabla ya kuondoka kuelekea Israeli, Rubio alionya dhidi ya hatua hiyo ya Knesset, akisema kuwa kupitishwa kwa mswada wowote wa aina hiyo kunaweza kuhatarisha usitishaji vita uliopo Gaza na kuleta matokeo yasiyo na tija kwa pande zote mbili.
Gazeti The Wall Street Journal liliripoti kwamba ongezeko la ziara za maafisa wa Marekani nchini Israeli linalenga kuhakikisha mwendelezo wa makubaliano ya kusitisha vita Gaza na kuzuia kuzuka kwa mivutano mipya ambayo inaweza kudhoofisha juhudi za kidiplomasia zinazoendelea.
Makamu wa Rais Vance alikamilisha ziara yake Alhamisi baada ya kufanya kikao cha ngazi ya juu na makamanda wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Israeli katika makao makuu ya Wizara ya Ulinzi mjini Tel Aviv, ambapo walijadili maendeleo ya uratibu wa shughuli za kijeshi katika Ukanda wa Gaza.
Wakati wa mkutano wake na Makamu wa Rais wa Marekani mjini Yerusalemu siku ya Jumatano, Rais wa Israeli Isaac Herzog alisisitiza umuhimu wa kuimarisha matumaini miongoni mwa Waisraeli na Wapalestina, na kuhimiza juhudi za pamoja za kurejesha amani ya kudumu.
Kwa upande wake, Vance alisema kuwa Marekani na Israeli zinaendelea kushirikiana kuimarisha usitishaji vita Gaza na kufungua tena baadhi ya miundombinu muhimu.
Alionyesha matumaini kuwa mpango wa amani wa Rais Trump utaendelea licha ya changamoto zilizopo, na hatimaye kuchangia katika kuimarisha utulivu na amani katika eneo hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli, Gideon Sa’ar, naye alisisitiza dhamira ya serikali yake kuhakikisha mafanikio ya mpango huo wa Gaza, akitoa wito kwa Hamas na Harakati ya Jihad ya Kiislamu kuacha mapigano na kuweka silaha zao chini.
Trump asitisha mazungumzo ya kibiashara na Canada: Kunani?

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha mara moja mazungumzo yote ya kibiashara na Canada, akitaja tangazo la televisheni lililomtumia sauti ya Rais wa zamani Ronald Reagan akipinga sera za ushuru kama kichocheo cha uamuzi huo.
Kupitia chapisho kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema tangazo hilo, lililodhaminiwa na serikali ya jimbo la Ontario, limeonyesha “mwenendo wa kukera” unaolenga kuingilia masuala ya ndani ya Marekani.
“Kwa kuzingatia tabia yao isiyokubalika, MAZUNGUMZO YOTE YA KIBIASHARA NA KANADA YAMEKOMA KUANZIA SASA,” aliandika Trump Alhamisi usiku.
Rais huyo ameweka kodi ya asilimia 35 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Kanada, ingawa ameidhinisha msamaha kwa bidhaa fulani zilizo chini ya Makubaliano ya Biashara Huria ya Amerika Kaskazini (USMCA) mkataba wa kibiashara kati ya Marekani, Kanada na Mexico alioufanyia marekebisho katika muhula wake wa kwanza.
Trump alieleza kuwa video hiyo imelenga “kuathiri maamuzi ya Mahakama Kuu ya Marekani”, ikizingatiwa kuwa mwezi Novemba mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi muhimu kuhusu uhalali wa sera zake pana za ushuru wa kimataifa.
Uamuzi huo unatazamiwa kuwa mtihani mkubwa zaidi wa mamlaka ya urais na sera za kiuchumi za Trump, ambao unaweza kulazimisha serikali ya Marekani kurejesha mabilioni ya dola zilizokusanywa kupitia ushuru huo.
Tangazo hilo la dakika moja, lililotolewa wiki iliyopita, linaonyesha picha za Soko la Hisa la New York na mitambo ya mizigo iliyopeperusha bendera za Marekani na Canada, huku sauti ya Reagan ikisikika akizungumza.
Sehemu hiyo imenukuliwa kutoka hotuba ya redio ya kitaifa ya mwaka 1987, ambapo Reagan alijadili athari za sera za kibiashara za kulinda soko la ndani.
“Wakati mtu anaposema ‘tuiweke ushuru kwa bidhaa kutoka nje,’ huonekana kana kwamba anafanya jambo la kizalendo kwa kulinda bidhaa na ajira za Marekani. Na mara nyingine, hufanya kazi kwa muda mfupi tu,” alisema Reagan.
“Lakini kwa muda mrefu, vizuizi kama hivyo vya biashara huumiza kila Mmarekani, na mfanyakazi. Ushuru wa juu huleta kulipizana kisasi kutoka mataifa mengine, na kuanzisha vita vya kibiashara vinavyoporomosha masoko, kufunga biashara na viwanda, na kuacha mamilioni bila ajira.”
Kupitia chapisho kwenye X (zamani Twitter), Shirika la Ronald Reagan Foundation lililaani matumizi ya sauti na video ya Reagan bila ruhusa, likisema serikali ya Ontario “ilitumia kwa kuchagua na kuhariri” sehemu za hotuba hiyo kwa njia inayopotosha ujumbe wake wa asili.
“Serikali ya Ontario haikuomba wala kupata ruhusa ya kutumia na kubadilisha hotuba hiyo,” ilisomeka taarifa ya shirika hilo, likiongeza kwamba linaendelea kuchunguza hatua za kisheria dhidi ya tukio hilo.
Shirika hilo lilisisitiza kuwa tangazo hilo limepotosha nia halisi ya Reagan, likionyesha wasiwasi kwamba matamshi ya kiongozi huyo wa zamani yametumiwa vibaya kwa malengo ya kisiasa.
Marekani yauwa watatu katika shambulizi la pili dhidi ya boti zinazodaiwa kuwa za dawa za kulevya huko Pasifiki

Rais wa Marekani Donald Trump amesema utawala wake uko vitani na magenge ya wahalifu wanaosafirisha madawa ya kulevya na watu kuelekea Marekani na kusema watawaua watu hao.
Mashambulizi ya hivi punde yanayofanywa na Marekani katika pwani ya Carribean yamewaua takriban watu arobaini wanaoshukiwa kuwa wasafirishaji madawa ya kulevya kwa kutumia boti.
Akikashifu hatua hizo za Marekani,Rais wa Colombia Gustavo Petro amesema vifo vinazidi kuongezeka.
Mashambulizi hayo ya angani yanayofanywa na Marekani yametajwa na wanasheria wengi na asasi za kiraia kuwa mauaji ya kiholela.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.