Starmer kutoa wito Ukraine kuongezewa makombora na Ulaya

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer(kushoto) akiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy (kulia)Picha: Suzanne Plunkett/REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atatoa mwito kwa viongozi wa Ulaya kuongeza msaada wa makombora ya masafa marefu kwa Ukraine katika mkutano wa kilele utakaofanyika mjini London Ijumaa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy atakuwa mmoja wa watakaohudhuria mkutano huo wa kilele.

Katika taarifa, afisi ya Starmer imesema mwito wake huo atakaoutoa katika mkutano huo uliopewa jina “muungano wa walio na nia” unalenga kuhakikisha kuwa Ukraine imekuwa na mwendelezo wa mafanikio iliyoyapata wiki hii katika uwanja wa mapambano.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen na mwenzake wa Uholanzi Dick Schoof wanatarajiwa pia kuhudhuria mkutano huo wa kilele London huku viongozi wengine akiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakitarajiwa kujiunga kwa njia ya mtandao.

Wandani wa ukraine wiki hii wameiwekea Urusi shinikizo zaidi huku Marekani ikitangaza vikwazo vikali dhidi ya sekta ya mafuta ya Urusi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment