Oxfam: Zaidi ya watu milioni 21 wahitaji msaada Kongo

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wawasili katika kambi za muda huko Rugerero mnamo Januari 28, 2025Picha: TONY KARUMBA/AFP

Zaidi ya watu milioni 21 wanahitaji msaada wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hii ikiwa idadi ya karibu humusi moja ya watu. Haya ni kwa mujibu wa shirika la Oxfam nchini Ufaransa.

Shirika hilo limesema Kongo inakabiliwa na mojawapo ya majanga makubwa na yaliyosahaulika ya kibinadamu duniani na kwamba hali inaendelea kuwa mbaya zaidi.

Oxfam, pia imesema unyanyasaji wa kijinsia umefikia viwango vya kutisha, huku mwanamke mmoja akibakwa kila baada ya dakika nne.

Msaada wa kimataifa wapungua

Hata hivyo licha ya hali hiyo ya dharura, msaada wa kimataifa unapungua.

Oxfam, imesema katika muda wa mwaka mmoja, ufadhili wa misaada muhimu umepungua kwa thuluthi mbili nchini Kongo na imelihimiza kongamano la kimataifa kuhusu Kanda ya Afrika ya Maziwa Makuu, linaotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa Oktoba 30, kuchukuwa hatua zaidi ya matamko ya nia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment