Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UN ( Kushoto) na mwenzake wa Marekani Donald Trump ( Kulia)Picha: Ministry of Communications/ZUMA/IMAGO
Waziri wa Muungano wa Korea Kusini, Chung Dong-young, ametoa wito kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, kukutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ziara yake ijayo barani Asia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Yonhap, Chung amesema ziara ya Trump nchini Korea Kusini ni “fursa kutoka mbinguni” ambayo inaweza kusaidia kuinua hadhi ya Korea Kaskazini kimataifa na kuboresha uchumi wake.
Ameongeza kuwa ziara hiyo inaweza kurahisisha mazungumzo kati ya Trump na Kim bila urasimu wa kawaida unaochelewesha mashauriano kama hayo.
Trump anatarajiwa kuanza ziara ya siku tano barani Asia, ambapo atazitembelea Malaysia, Japan na Korea Kusini, ikiwa ni ya kwanza katika kanda hiyo tangu kurejea madarakani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.