Usiseme kila Kitu….Wanaweza wakaiba wazo lako ila hawawezi kuiba neema yake.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Sio kila KITU KIZURI kinachokupa FURAHA unatakiwa UKIONESHE…

Wanadamu wana tabia ya KUHARIBU vyanzo vya vile vinavyokupa FURAHA.

Jifunze kuwa na KIASI katika KUONYESHA…

…au KUSEMA kile ambacho ndio hasa CHANZO chako cha furaha.

Sio kila MTU ANATAKIWA AKIJUE na sio kila mtu anatakiwa AKISIKIE…

…chagua wa KUMWAMBIA.

Usisahau kuwa watu hawawezi KUHARIBU wasichokijua.

Kuna “levels” mbalimbali: Kuna mambo ni yako peke yako.

Kuna mengine ni yako wewe na mwenzako…

Kuna mengine ni yako wewe na watu wachache…

Na kuna yale ambayo ni ya kila mtu anaweza kuyajua (Public)…

Ukichanganya ukayasema/kuonyesha yale yanayopaswa yawe ya siri…

…utakuwa umekaribisha changamoto ambayo inaweza kuwa ndio chanzo cha kupoteza furaha yako.

Usisahau kuwa, sio kila anayekuona una furaha anatamani uendelee kuwa na furaha siku zote, Be Wise!

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment