Uingereza yachunguza visa vya wasichana wenye umri mdogo wanaorubuniwa kujidhuru

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mhalifu wa mtandaoni

Mamlaka ya kitaifa ya Uingereza ya kukabiliana na uhalifu imesema inachunguza ongezeko la visa vinavyohusisha makundi ya vijana wanaowalenga wasichana wenye umri mdogo kwa lengo la kuwarubuni kujidhuru.

Makundi hayo ya vijana yanatumia mitandao ya kijamii kutafuta wasichana wanaoposti kuhusu matatizo yao hasa ya kuhangaika kiakili,kujifanya kuwa wanataka urafiki nao kisha kuwashawishi kujidhuru au kufanya vitendo vya kujidhalilisha mubashara katika mitandao hiyo ya kijamii.

Mamlaka hiyo ya kukabiliana na uhalifu inasema inatiwa wasiwasi na ongezeko hilo la vitisho na uhalifu mitandaoni.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment