Rubio: Kuzingira Ukingo wa Magharibi kunatishia amani Gaza

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani, Marco RubioPicha: Ross D. Franklin/AP Photo/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, ameionya Israel dhidi ya kuuzingira Ukingo wa Magharibi.

Rubio amesema hatua zilizochukuliwa na bunge la Israel pamoja na ghasia za walowezi kwenye eneo hilo, zinatishia mkataba wa amani wa Gaza.

Mnamo Jumatano, wabunge wa Israel walipitisha miswada miwili ya kuuzingira Ukingo wa Magharibi.

Hatua hiyo imejiri wiki moja tu tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango wa Rais Donald Trump wa usitishaji vita na unaolenga kumaliza kabisa mzozo kati ya Israel na Hamas, ambao umedumu sasa kwa miaka miwili.

Huko the Hague, Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, imesema ni sharti Israel iliruhusu Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina Gaza (UNRWA), kuendelea na shughuli zake za kiutu.

Rais wa mahakama hiyo Yuji Iwasawa amesema Israel ina jukumu la kukubali na kuweka mazingira mazuri ya mashirika ya misaada kufanya shughuli zake. Israel haijairuhusu UNRWA kuingiza misaada tangu mwezi Machi, ila shirika hilo linaendelea kuendesha vituo vya matibabu, huduma za usafi na shule kwa watoto Gaza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment