Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Wachezaji wa Frankfurt Fares Chaini na Robin KochPicha: Canales Carvajal/dpa/picture alliance
Eintracht Frankfurt ilipewa funzo la kandanda usiku wa kuamkia Alhamis mjini Frankfurt kwa kucharazwa mabao 5-1 na Liverpool ya England katika mechi ya ligi ya vilabu bingwa Ulaya.
Ushindi huo kwa Liverpool umefikisha mwisho msururu wao wa kupoteza mechi nne mfululizo katika mashindano yote ila ulitiliwa doa na majeraha kwa wachezaji wao muhimu Alexander Isak na Jeremie Frimpong.
Kiungo mbunifu wa timu ya taifa ya Ujerumani Florian Wirtz aling’aa katika mechi hiyo kwa kutoa pasi muhimu zilizopelekea kupatikana kwa mabao ya Cody Gakpo na Dominik Szoboszlai.
Kwengineko mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich walikuwa na kazi rahisi uwanjani kwao Allianz Arena walipowalaza Club Brugge mabao 4-0 Lennart Karl, Harry Kane, Luis Diaz na Nicholas Jackson wakiwa wafungaji wa mabao hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.