Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali KhameneiPicha: Office of the Iranian Supreme Leader/AP/picture alliance
Iran imetahadharisha kuhusu mashambulizi mapya ya kijeshi dhidi yake na kusema ‘yatashindwa tena’.
Tahadhari hiyo imetolewa baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia nishati ya Atomiki kuelezea hofu ya uwezekano wa ‘matumizi mapya ya nguvu’ ikiwa juhudi za kidiplomasia na Tehran zitagonga mwamba.
Mnamo katikati ya Juni, Israel ilifanya mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya Iran, na kusababisha vita ambapo Iran ilijibu kwa makombora na droni.
Wakati wa mzozo huo wa Israel na Iran, vita hivyo vilivyodumu kwa siku 12, Israel ilishambulia vituo vya kijeshi na vya nyuklia vya Iran huku Marekani ikijiunga baadaye kwa kushambulia vinu vikuu vya nyuklia.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.