Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Kanda ya sahel ni miongoni mwa maeneo yanayozongwa na mizozo ya silaha barani AfrikaPicha: Nic Bothma/dpa/picture alliance
Takriban asilimia 40 ya mizozo inayohusu zana za kivita inatokea bara la Afrika.
Makamu Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Gilles Carbonnier ameeleza kuwa kwa sasa, kuna takriban mizozo 50 ya silaha inayoendelea barani humo.
Hiyo inaashiria ongezeko la asilimia 45 tangu mwaka 2020 na hivyo kuiweka mizozo ya Afrika kuwa asilimia 40 ya mizozo yote ya silaha ulimwenguni.
Miongoni mwa nchi zinazozongwa na mizozo ya silaha ni kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan, Mali na Niger
Bara hilo lina takriban watu bilioni 1.4, na lina utajiri wa madini na idadi kubwa ya vijana. Lakini sehemu nyingi ya bara hilo zimekumbwa na umaskini na ukosefu wa usalama.
Kulingana na Carbonnier, mizozo hiyo imesababisha watu milioni 35 kuyakimbia makaazi yao, hiyo ikiwa takriban nusu ya wahamiaji wote ulimwenguni.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.