Wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika 2025 wajulikana

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah akitia mpira wavuniPicha: Roger Evans/picture-alliance/Action Plus/dpa

Mshambuliji wa Liverpool Mohamed Salah na beki wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi ni miongoni mwa nyota 10 walioteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa 2025, waandaaji wa tuzo hiyo Afrika CAF wametangaza.

Mshambuliji wa Liverpool Mohamed Salah na beki wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi ni miongoni mwa nyota 10 walioteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa 2025, waandaaji wa tuzo hiyo shirikisho la soka Afrika CAF limetangaza hii leo.

Salah alimaliza wa nne na Hakimi wa sita katika tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya  Ballon d’Or ya 2025. Salah amewahi kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka mara mbili huku nahodha wa Morocco, Hakimi akiitafuta tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.

Katika orodha hiyo ni wachezaji wawili tu ambao wanacheza katika ligi ya ndani ya bara la Afrika, wachezaji hao ni raia wa Kongo, Fiston Mayele kutoka klabu ya Pyramids FC ya Misri na  Oussama Lamlioui anayechezea RS Berkane ya Morocco.

Mshindi wa mara ya mwisho wa tuzo hiyo Mnigeria Ademola Lookman, hayupo kwenye orodha hiyo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment