Uganda ishinikizwe kufuta sheria dhidi ya ushoga

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Ofisi za Benki ya Dunia jijini Washington, MarekaniPicha: ullstein bild – Fotoagentur imo

Shirika la Kimataifa la Amnesty limeitaka Benki ya Dunia kuishinikiza serikali ya Uganda kufuta sheria kali dhidi ya watu wanashiriki mapenzi ya jinsia moja kabla ya kurejeshwa tena kwa ufadhili uliokuwa umesitishwa.

Wito wa Amnesty umetolewa baada ya Afisa mmoja wa wizara ya fedha nchini Uganda kusema mapema wiki hii kwamba nchi hiyo itapokea kwa muda wa miaka mitatu jumla ya dola bilioni 2 kutoka kwa  Benki ya Dunia  ambayo ilisitisha mikopo yote kwa Uganda baada ya rais Yoweri Musevi kusaini mwaka 2023 sheria hiyo dhidi ya jamii ya LGBTQ+.

Wakati huo Benki ya Dunia ilisema kuwa miradi yote inayoifadhili inapaswa kuzingatia sera zake zisizo za kibaguzi. Sheria ya  Uganda dhidi ya ushoga ni mojawapo ya sheria kali zaidi duniani ikijumuisha wakati mwengine hukumu ya kifo katika baadhi ya matukio.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment