Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Hii imekuwa changamoto kubwa katika Biashara/Kampuni nyingi, wafanyakazi wanafanya wanavyotaka …
USIVUMILILIE MAKOSA HAYA…
1. KUCHELEWA KAZINI BILA SABABU YA MSINGI.
Kuchelewa mara kwa mara kunapunguza tija na kuathiri utaratibu wa kazi. Wateja au wenzake wanaweza kuanza kupoteza imani kwa huduma zako.
SULUHISHO:Weka kanuni thabiti za muda wa kufika kazini. Tumia mfumo wa kurekodi saa za kuingia na kutoka, na toa onyo au adhabu kwa wanaochelewa bila sababu halali.
2. KUJIBU VIBAYA AU KWA UKOSEFU WA HESHIMA KWA WATEJA.
Mteja akihisi kudharauliwa, si tu atapotea, bali pia atawashauri wengine wasitumie huduma zako.
SULUHISHO:Toa mafunzo ya huduma kwa wateja. Wahimize wafanyakazi kutabasamu, kusikiliza, na kuomba msamaha wanapokosea.
3. KUVAA MAVAZI YASIYOFAA KAZINI
Muonekano wa mfanyakazi una athari kubwa kwa taswira ya biashara. Wateja wanajenga imani kupitia mwonekano wa kwanza.
SULUHISHO:Weka kanuni za mavazi (dress code). Eleza ni mavazi gani yanayokubalika kulingana na aina ya biashara yako.
4. KUTOKUWA NA HESHIMA KWA MWAJIRI AU WENZAKE
Ukosefu wa heshima hujenga mazingira mabaya ya kazi, migogoro, na kushusha morali ya timu.
SULUHISHO:Jenga utamaduni wa kuheshimiana. Toa onyo mapema kwa mfanyakazi asiyeonyesha heshima, na ikiendelea, chukua hatua za kinidhamu.
5. KUKOSA UWAJIBIKAJI KATIKA MAJUKUMU
Mfanyakazi asiyejua wajibu wake au asiyejituma huchelewesha maendeleo ya biashara.
SULUHISHO:Weka malengo ya wazi na tathmini za utendaji (performance review). Toa maoni ya kujenga na motisha kwa wanaotekeleza vizuri.
6. KUSAMBAZA MANENO AU TAARIFA ZA UONGO KUHUSU BIASHARA
Kusambaza maneno mabaya ndani au nje ya biashara kunaharibu jina na uaminifu wa kampuni.
SULUHISHO:Eleza madhara ya tabia hii waziwazi. Weka sera ya nidhamu kali kwa yeyote atakayehusika na uzushi au fitina kazini.
7. KUJARIBU KUPANDA KICHWA AU KUTAKA KUTAWALA MWAJIRI.
Baadhi ya wafanyakazi wakisha jifunza mambo machache huanza kudharau mwajiri au kutaka kufanya maamuzi bila ruhusa.
SULUHISHO:Weka mipaka ya wazi ya majukumu na mamlaka. Kumbusha kila mtu umuhimu wa heshima na utiifu wa kikazi. Ikiwezekana, mpe majukumu yanayompa nafasi ya kutumia ujuzi wake bila kuvuka mipaka.
Ni jambo gani bado linakusumbua kwenye biashara yako kuhusu Wafanyakazi?
Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.
Share ujumbe huu kwa waajiri wengine ili kuweza kupata mafanikio makubwa kwenye biashara zao.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.