Korea Kaskazini yafyetua makombora kabla ya mkutano wa APEC

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Televisheni ya Korea Kaskazini ikionyesha zoezi la ufyetuaji wa komboraPicha: Jung Yeon-je/AFP

Jeshi la Korea Kusini limesema Korea Kaskazini imefyetua makombora kadhaa ya masafa marefu kuelekea baharini bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi. Hii ni kabla ya mkutano wa kilele wa APEC utakaofanyika Korea Kusini.

Haya yanajiri siku chache kabla ya Korea Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia-Pasifiki,  APEC.

Mkutano huo utafanyika wiki ijayo katika mji wa Gyeonju na kuhudhuriwa na marais Donald Trump wa Marekani na yule wa China Xi Jinping pamoja na viongozi wengine wa ulimwengu.

Awali wataalamu walisema  Korea Kaskazini  inaweza kufanya majaribio ya uchochezi kwa kufyetua kombora kabla au wakati wa mkutano huo wa kilele wa APEC ili kusisitiza azma ya nchi hiyo kutambulika kama taifa lenye silaha za nyuklia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment