Zelensky alenga kununua mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akitoa hotuba yake mjini KievPicha: Ukrainian Presidential Press Service/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi yake inajiandaa kununua mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot.

Uamuzi wa Zelensky ni baada ya kushindwa wiki iliyopita kumshawishi rais wa Marekani Donald Trump kumpatia makombora ya masafa marefu ya Tomahawk.

Katika hotuba yake ya video Jumatatu usiku,  Zelensky amesema alipokuwa Washington alizungumza na watengenezaji wa silaha hizo na wakaonyesha utayari wa kushirikiana na Ukraine lakini akasisitiza kuwa upatikanaji wa mifumo hiyo ya ulinzi wa anga si jambo rahisi, lakini ni moja ya hakikisho la usalama itakayosaidia kwa muda mrefu.

Hata hivyo Zelensky alisifu mkutano wake na  Trump  licha ya kauli ya rais huyo wa Marekani kusema hapo jana kuwa haamini ikiwa Ukraine itashinda vita dhidi ya Urusi, ingawa hajaondoa kabisa uwezekano huo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment