Uganda kufanya uchaguzi mkuu Januari 15

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: SIMON MAINA/AFP/Getty Images

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imetangaza leo kuwa uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika Januari 15.

Rais aliyeko madarakani kwa sasa Yoweri Museveni atatafuta kuongeza muda wa utawala wake hadi kufikia karibu nusu karne katika uchaguzi huo.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa 2021, mpinzani mkuu wa Museveni anatarajiwa kuwa Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Wine anasema Museveni alishinda uchaguzi uliopita kutokana na wizi wa kura na vitisho kwa wapiga kura, madai yanayokanushwa na maafisa wa chama tawala cha NRM, wanaosema Museveni alishinda kihalali kutokana na uungwaji mkono aliokuwa nao.

Akiwa rais wa nne Afrika aliyehudumu kwa muda mrefu, Museveni na serikali yake wameifanyia mageuzi katiba ya Uganda na kuondoa ukomo wa umri na kuwa madarakani. Amekuwa madarakani tangu 1986.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment