Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akiwasili Mahakamani jijini ParisPicha: Stephanie Lecocq/REUTERS
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anatarajiwa Jumanne kwenda jela ya “la Santé” iliyopo katikati mwa mji mkuu Paris kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.
Mwezi Septemba, mahakama ya Ufaransa ilimkuta Sarkozy na hatia ya kula njama za uhalifu katika kesi inayohusiana na juhudi zake za kujipatia fedha kinyume cha sheria ili kufadhili kampeni yake ya uchaguzi wa mwaka 2007, fedha zilizotoka kwa mtawala wa Libya wakati huo Muammar Gaddafi.
Nicolas Sarkozy ambaye atakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa na hata katika Umoja wa Ulaya kwenda jela, alipokelewa wiki iliyopita na rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysée, lakini mazungumzo yao hayakuwekwa wazi. Mawakili wa Sarkozy aliyeiongoza Ufaransa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012, wametangaza kuwa watawasilisha mara moja ombi la kuachiliwa kwake.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.