Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Wapiganaji waKihouthi wa Yemen wakiwa katika maandamano mjini SanaaPicha: Osamah Yahya/dpa/picture alliance
Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wanawashikilia wafanyakazi wapatao 20 wa Umoja wa Mataifa, baada ya kuvamia kituo kingine cha taasisi hiyo ya kimataifa katika mji mkuu wa Yemen – Sanaa.
Ofisi ya mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen , imesema wafanyakazi hao akiwemo mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF nchini Yemen, wanazuiliwa katika kituo kilichopo katika kitongoji cha Hada kusini magharibi mwa mji wa Sanaa.
Umoja wa Mataifa umesema unawasiliana na kundi hilo la waasi pamoja na wadau wengine ili kujaribu kutafutia suluhu tatizo hilo na kurejesha udhibiti kamili wa vituo vyake huko Sanaa.
Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakiwashutumu bila ushahidi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuwa majasusi wa Marekani na Israel, shutuma zinazokanushwa na Umoja wa Mataifa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.